Home Uncategorized JESHI LA POLISI TANZANIA LAMUAGA RASMI SIRRO

JESHI LA POLISI TANZANIA LAMUAGA RASMI SIRRO

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi Nchini limemuaga rasmi aliyekuwa Mkuu wa Jeshi hilo Simon Nyankoro Sirro baada ya kumaliza utumishi wake katika Jeshi hilo.

Akiongea na waandishi wa habari leo mei 10 2023 katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam DPA Sirro amesema anamshukuru Mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini kipindi chote alichokuwa Mkuu wa Jeshi hilo.

IGP Mstafu Balozi Simon Sirro amebainisha kuwa katika utumishi wake atakumbuka mambo Mengi ambayo yalimuumiza kichwa ikiwemo la kuuwawa kwa askari tisa eneo la kibiti Mkoani Pwani.

Sambamba na hilo amewashukuru maafisa na askari wa vyeo mbalimbali katika Jeshi la Polisi Nchini kwa Mchango wao Mkubwa ambapo amesema walishirikiana kuhakikisha wanalinda raia na mali zao katika kipindi alicho ongoza Jeshi hilo.

Pia amevishukuru vyombo vya ulinzi na usalama kwa namna walivyo shirikiana katika kudhibiti uhalifu Nchini.

Vile vile amevishukuru vyombo vya habari na waandishi wa habari kwa namna alivyoshirikiana na vyombo hivyo kuwa hanarisha wananchi maganikio ya kudhibiti uhalifu Nchini.

Mwisho Mheshimiwa Balozi Sirro amewakaribisha watanzania kufika Mchini zimbambwe na kutangaza fulsa mbalimbali zilizopo Nchini Tanzania.

Previous articleJE UNAFAHAMU MAANA NA UMUHIMU WA RANGI NYEKUNDU KATIKA TIMU ZA SOKA?
Next articleMAWAZIRI WATATU WAJADILI UWEKEZAJI NA KILIMO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here