Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Mkoani Tabora , imenunua pikipiki 25 zenye thamani ya milion 69 na kiwapatia maafisa watendaji wa kata kwa ajili ya kuraisisha utoaji huduma za Kiutawala kwa wananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kaliua Jerry Mwanga ofisini kwake alisema kwamba pikipiki hizo zitaraisisha usimamizi wa miradi mbalimbali ya serikali inayotekelezwa wilayani humo.
Alisema kwamba maafisa hao baada ya kupewa pikipiki hizo wataweza kufuatilia kwa ukaribu marejesho ya mikopo kwa vikundi vilivyo ndani ya kata husika.
Aidha Mkurugenzi alisema wataweza kuendeleza na kuboresha mazingira ya utendaji katika maeneo yao na itawarahisishia kuwafikia kila mtu aliochukua mkopo katika halmashauri hiyo.
Hata hivyo Mwanga alibainisha kwamba maafisa watendaji hao katika mwaka wa fedha 2022/2023 , halmashauri imepanga kutenga fedha kwa ajili ya ofisi za kata ikiwa ni pamoja na matengenezo ya pikipiki zao.
Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batrida Buriani aliwakabidhi watendaji yao na kutoa maelekezo juu ya vyombo vya moto na matumizi sahihi wakati wanapokuwa barabarani na jinsi ya kuwafikia watu waliokopa mikopo katika halmashauri hiyo.
Alisema kwamba pikipiki hizo walizozipata ni kwa ajili ya usimamizi wa miradi inayotekelezwa katika maeneo yao na wazitunze ili ziweze kufanyakazi kwa muda mrefu.
Mkuu huyo wa mkoa alisema anatarajia pikipiki hizo , maafisa watendaji watakwenda kuboresha mazingira ya kazi ya kiutendaji ili kuleta chachu katika maelekezo waliopewa na halmashaur ya Kaliua.
Alisema kwamba kutokana na ukubwa wa wilaya hiyo , maafisa watendaji kata wamekuwa wakikabiiliwa na changamoto ya mazingira magumu katika utendaji wao hasa katika maeneo ya usimamizi wa miradi na ufuatiliaji wa maswala ya kiutawala.
Mkuu huyo wa mkoa aliwaasa mafisa watendaji hao wazitumie pikipiki hizo kwa uangalifu mkubwa na kufuata maelekezo waliopewa hasa wanapokwenda kwenye miradi na kuwafuatilia wadeni wa mikopo pale walipo kwa kutumia lugha nzuri.
Mwisho.