Mwandishi wetu Dar,
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amewataka Viongozi wa Shirikisho la Afrika la mchezo wa Mpira wa Miguu kwa Watu wenye Ulemavu (FAAF) pamoja Makamu wa Rais wa Shirikisho la dunia (WAFF) Bw. Mateus Widlock kufikiria kombe la dunia lijalo baada ya 2022 nchini Uturuki kuwa Tanzania.
Kuli hiyo ameitoa leo wakati wa hotuba yake kabla ya kufungua Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Viongozi wa Shirikisho la mchezo huo Afrika unaofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere Jijini Dar wa salaam.
“Tanzania iko tayari kuandaa Kombe la Dunia baada Uturiki 2022 naombeni mkalifikirie hilo,”Amesema Mhe. Bashungwa.
Hata hivyo katika hafla hiyo Mhe. Bashungwa aliongozana na Mtendaji wake katika Wizara yake, Dkt. Hassan Abbasi, Mkurugenzi wa Michezo Yusuph Singo Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Bi.Neema Msitha.
Ameutaka uongozi huo kuifikiria Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano hayo kutokana na mazingira bora yaliyowekwa chini ya Rais wa awamu ya sita inayoongozwa Mama shupavu Samia Suluhu Hassan.
Aidha, Mhe. Bashungwa ameeleza kuwa, dunia haina budi kujifunza kupitia mashindano hayo kwa kuondokana na mila potofu za ubaguzi na kuwaona watu wenye ulemavu ni binadamu kama walivyo wengine kwa kupewa haki sawa.
Kupitia tukio hilo Waziri Bashungwa ameyakaribisha mataifa yote kuja kutembelea vivutio adhimu vilivyopo Tanzania ukiwemo Mlima Kilimanjaro pamoja mbunga mbalimbali za wanyama.
Awali Mhe. Bashungwa amewashukuru wajumbe hao kwa salama nyingi zenye sifa nyingi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu kwa uongozi mahiri na Imara unaojali makundi yote na kwa uratibu makini wa mashindano hayo.
Kwa wake Rais wa Shirikisho hilo wa Afrika (FAAF) Richard Nii Adesah ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano na uwezeshaji wa mashindano hayo katika kipindi chote na itasaidia kuleta mabadiliko makubwa kwenye michezo ya walemavu Barani Afrika.