Home SPORTS TANZANIA IKO TAYARI KUANDAA KOMBE LA DUNIA BAADA YA UTURUKI 2022

TANZANIA IKO TAYARI KUANDAA KOMBE LA DUNIA BAADA YA UTURUKI 2022

 Mwandishi wetu Dar,

WAZIRI  wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amewataka Viongozi wa Shirikisho la Afrika la mchezo wa Mpira wa Miguu kwa Watu wenye Ulemavu (FAAF)   pamoja  Makamu wa Rais wa Shirikisho la dunia (WAFF) Bw. Mateus Widlock kufikiria kombe la dunia lijalo baada ya 2022 nchini Uturuki kuwa Tanzania.

Kuli hiyo ameitoa leo wakati wa hotuba yake kabla ya kufungua Mkutano Mkuu wa  Uchaguzi wa Viongozi wa Shirikisho la mchezo huo Afrika unaofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere Jijini Dar wa salaam.

“Tanzania iko tayari kuandaa Kombe la Dunia baada Uturiki 2022 naombeni mkalifikirie hilo,”Amesema Mhe. Bashungwa.

Hata hivyo katika hafla hiyo Mhe. Bashungwa  aliongozana na Mtendaji wake katika Wizara yake, Dkt. Hassan Abbasi, Mkurugenzi wa Michezo Yusuph Singo Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Bi.Neema Msitha.

Ameutaka  uongozi huo kuifikiria Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano hayo  kutokana na mazingira bora yaliyowekwa chini ya Rais wa awamu ya sita inayoongozwa Mama shupavu Samia Suluhu Hassan.

Aidha, Mhe. Bashungwa ameeleza kuwa, dunia haina budi kujifunza kupitia mashindano hayo kwa kuondokana na mila potofu za ubaguzi na kuwaona watu wenye ulemavu ni binadamu kama walivyo wengine kwa kupewa haki sawa.

Kupitia tukio hilo Waziri Bashungwa ameyakaribisha mataifa yote kuja kutembelea vivutio adhimu vilivyopo Tanzania ukiwemo Mlima Kilimanjaro pamoja mbunga mbalimbali za wanyama.

Awali Mhe. Bashungwa amewashukuru wajumbe hao kwa salama nyingi zenye sifa nyingi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu kwa uongozi mahiri na Imara unaojali makundi yote na kwa uratibu makini wa mashindano hayo.

Kwa wake Rais wa Shirikisho hilo wa Afrika (FAAF) Richard Nii Adesah ameipongeza  Serikali ya Tanzania kwa  ushirikiano na uwezeshaji wa mashindano hayo katika kipindi chote na itasaidia kuleta mabadiliko makubwa  kwenye michezo ya walemavu Barani Afrika.

 

Previous articleKIDUNDA AMTAKA KATOMPA AJIPANGE DISEMBA 26
Next articleALIYOYASEMA KAMISHNA JENERALI DCEA GERALD KUSAYA WAKATI AKIELEZA MAFANIKIO YA MAMLAKA HIYO MIAKA 60 YA UHURU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here