Na: Costantine James, Geita.
Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Buckreef imetoa milioni 420 kwa jamii kwa lengo la kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeo katika halmashauri ya wilaya ya Geita mkaoani humo.
Hafra ya utiaji saini ya makubaliano ya utekelezaji wa miradi hiyo imefanyika leo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita ambapo Kampuni hiyo imetoa pesa kwa ajili yakwenda kutekeleza miradi ya kimaendeleo katika halmashauri ya wilaya ya Geita ikwemo miradi ya elimu, afya na mazingira kama pesa za uwajibikaji wa makampuni kwa jamii (CSR).
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buckreef Gastoni Mujwahuzi amesema Mgodi huo ulianza kwa kuzalisha tani 15 kwa saa na sasa wanazalisha tani 45 huku wakitarajia kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2024 kuanza kuzalisha tani 90 hadi 100 kwa saa.
Amesema kwa kutambua wajibu wa shirika hilo kwa kushirikiana na jamii katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo hivyo wameamua kutoa milioni 420 kwa lengo la kushirikiana na jamii katika katika kutekeleza miradi ya kimaendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela ameupogeza Mgodi wa Buckreef kwa kutoa pesa hizo huku akizitaka kampuni za uchimbaji wa madini mkoani humo kutoa pesa hizo mapema kwa lengo la kuwezesha miradi hiyo kutekelezwa na kukamilika kwa wakati.
Shigela amewataka wale wote wanaohusika na usimamizi wa miradi hiyo kuhakikisha wanasimamia vyema kwa lengo la kuwezesha miradi hiyo kukamilika kwa wakati ili iweze kutumika kama ilivyokusudiwa.
Amesema ili kufanikisha ukamilishwaji wa miradi hiyo kwa wakati amewataka Buckreef kuhakikisha wanakamailisha michakato ya manunuzi kwa wakati ili kuondoa ucheleweshwaji wa miradi hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Geita Cornel Magembe amemhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Geita pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria hafra hiyo kuhakikisha atasimamia vyema miradi hiyo ili iweze kuleta tija kwa jamii.