NA: STELLA KESSY
MASHINDANO ya Riadha ya Kombe la Taifa ( Taifa Cup) yanatarajia kurindima leo kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa,Dar Es Salaam.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ,Yusuph Singo,mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar imethibitisha kushiriki.
” Kwa mara ya kwanza muda mrefu mikoa inayoshiriki mashindano haya imethibitisha kushiriki Michezo mbalimbali ikiwamo Mbio za Kati na relay itafanyika ,” alisema Singo.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi wa Mashindano hayo Jackson Ndaweka, alisema mikoa 24 imethibitisha kushiriki ambapo Kati ya hao 19 kutoka Tanzania Bara na mitano Zanzibar jumla ya wanariadha 280.
Amesema kuwa jumla ya michezo 18 itashindaniwa katika mashindano hayo .
Wakati huo huo hatua ya nusu fainali ya mashindano ya netiboli na Soka inatarajia kupigwa leo.
Kwa upande wa wanawake Dar Es Salaam imekuwa ya kwanza kukata tiketi ya nusu fainali baada ya kuichapa mabao 2-1 dhidi ya Mjini Magharibi katika mchezo uliochezwa jana ,Dar Es Salaam.
Wakati upande wa wanaume Mara na Mjini Magharibi zimefanikiwa kutinga nusu fainali katika hatua ya robo fainali ya mashindano ya Taifa cup uliyofanyika jana ,Dar Es Salaam.
Mara uliipata nafasi hiyo baada y kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Manyara,wakati na Mjini Magharibi imefanikiwa baada ya kuichapa mabao 3_ 0 dhidi ya Kusini Unguja.