Home SPORTS MASHINDANO YA RIADHA TAIFA CUP KUTIMUA VUMBI DAR

MASHINDANO YA RIADHA TAIFA CUP KUTIMUA VUMBI DAR


NA: STELLA KESSY

MASHINDANO ya Riadha ya Kombe la Taifa ( Taifa Cup)  yanatarajia kurindima leo  kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa,Dar Es Salaam.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ,Yusuph Singo,mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar imethibitisha kushiriki.

” Kwa mara ya kwanza  muda mrefu mikoa inayoshiriki mashindano haya imethibitisha kushiriki Michezo mbalimbali ikiwamo Mbio za Kati na relay itafanyika ,” alisema Singo.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi wa Mashindano hayo Jackson Ndaweka, alisema mikoa 24  imethibitisha kushiriki ambapo Kati ya hao 19 kutoka Tanzania Bara na mitano Zanzibar jumla ya wanariadha 280.

Amesema kuwa jumla ya michezo 18 itashindaniwa katika mashindano hayo .

Wakati huo huo hatua ya  nusu fainali ya mashindano ya netiboli na Soka inatarajia kupigwa leo.

Kwa upande wa wanawake Dar Es Salaam imekuwa ya kwanza kukata tiketi ya nusu fainali baada ya kuichapa mabao 2-1 dhidi ya Mjini Magharibi katika mchezo uliochezwa jana ,Dar Es Salaam.

Wakati upande wa wanaume Mara  na Mjini Magharibi zimefanikiwa kutinga nusu fainali katika hatua ya robo fainali ya mashindano ya Taifa cup uliyofanyika jana ,Dar Es Salaam.

Mara uliipata nafasi hiyo baada y kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Manyara,wakati  na Mjini Magharibi imefanikiwa baada ya kuichapa mabao 3_ 0 dhidi ya Kusini Unguja.
Previous articleTAIFA CUP ‘NETBALL’ YASHIKA KASI DAR
Next articleRWANDAMINA AJIUZULU UKOCHA AZAM
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here