Na.Alex Sonna, Dodoma
RAIS Samia Suluhu Hassan,amezindua kamati ya ushauri ya kitaifa kuhusu utekelezaji wa ahadi za nchi kwenye jukwaa la kizazi chenye usawa huku akitoa maagizo kwa Mawaziri,Wakuu wa Mikoa,Wakurugenzi pamoja na Taasisi zote za Wizara kuhakikisha wanatoa kipaumbele katika utekelezaji wa ahadi hizo.
Pia Rais Samia ametoa maagizo sita kwa Kamati hiyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha inatoa Ushauri bora namna ya ushirikishwaji wa Wadau wa kimkakati pamoja na kushiriki shughuli za utoaji Elimu kwenye jukwaa la usawa kwa wananchi.
Rais Samia ametoa maagizo hayo leo Desemba 16,2021 jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Kamati hiyo ambayo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali,Dini,Mabalozi vikiwemo Vyama vya siasa na wananchi.
Aidha Rais Samia ameiagiza kamati hiyo kusimamia na kuhakikisha ahadi za kuinua haki za kiuchumi kwa jamii hasa wanawake zinatekelezwa vyema na malengo yake yanafikiwa.
“Naamini wataalamu hawa katika kamati watanishauri vizuri ili kuweza kutekeleza ahadi zetu itakuwa aibu kama sisi ambao tumejiweka kuwa vinara tukashindwa na mataifa ambayo hajajiweka vinara ambayo ni mataifa yanayoendelea kama tulivyo sisi”alisema
Hata hivyo,ameziagiza sekta zote na taasisi kulipa kipaumbele suala la ahadi zilizotolewa na serikali kwenye jukwaa hilo la usawa wa kijinsia.
Credit – Fullshangwe Blog.
|