Home LOCAL RAIS SAMIA AZINDUA KAMATI YA USHAURI YA KITAIFA KUHUSU UTEKELEZAJI WA AHADI...

RAIS SAMIA AZINDUA KAMATI YA USHAURI YA KITAIFA KUHUSU UTEKELEZAJI WA AHADI ZA NCHI KWENYE JUKWAA LA KIZAZI CHENYE USAWA

 

Na.Alex Sonna, Dodoma

RAIS Samia Suluhu Hassan,amezindua  kamati ya ushauri ya kitaifa kuhusu utekelezaji wa ahadi za nchi kwenye jukwaa la kizazi chenye usawa huku akitoa maagizo kwa Mawaziri,Wakuu wa Mikoa,Wakurugenzi pamoja na Taasisi zote za Wizara kuhakikisha  wanatoa kipaumbele katika utekelezaji wa ahadi hizo.

Pia Rais Samia ametoa maagizo sita kwa Kamati hiyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha inatoa Ushauri bora namna ya ushirikishwaji wa Wadau wa kimkakati pamoja na kushiriki shughuli za utoaji Elimu kwenye jukwaa la usawa kwa wananchi.

Rais Samia ametoa maagizo hayo leo Desemba 16,2021 jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Kamati hiyo ambayo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali,Dini,Mabalozi vikiwemo Vyama vya siasa na wananchi.

Aidha  Rais Samia ameiagiza kamati hiyo kusimamia na kuhakikisha ahadi za kuinua haki za kiuchumi kwa jamii hasa wanawake zinatekelezwa vyema na malengo yake yanafikiwa.

“Naamini wataalamu hawa katika kamati watanishauri vizuri ili kuweza kutekeleza ahadi zetu itakuwa aibu kama sisi ambao tumejiweka kuwa vinara tukashindwa na mataifa ambayo hajajiweka vinara ambayo ni mataifa yanayoendelea kama tulivyo sisi”alisema

Hata hivyo,ameziagiza sekta zote na taasisi kulipa kipaumbele suala la ahadi zilizotolewa na serikali kwenye jukwaa hilo la usawa wa kijinsia.

Credit – Fullshangwe Blog.

Previous articleWAZIRI WA MAJI KUZINDUA MIRADI YA MAJI RUKWA
Next articleABU DHABI YAAHIDI KUENDELEA KUIPIGA JEKI TANZANIA KIMAENDELEO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here