Na: Dotto Mwaibale, Singida
SHEIKH wa Mkoa wa Singida, Issa Nasoro amepiga marufuku wasanii mkoani hapa kuacha mara moja tabia ya kuchezea alama za dini kwa lengo la kutafuta umaarufu (kiki)
Nassoro ameyasema hayo wakati akizungumza na Waumini wa dini ya kiislam katika dua ya hauli ya Sheikh Nassoro Issa Salum Alharith Alqadirii Baba wa Sheikh Issa Nassoro iliyofanyika kwenye Msikiti wa Muhajirina uliopo Majengo Manispaa ya Singida Aprili 7, 2023 na baada ya hapo alifuturisha mamia ya waislam nyumbani kwake futari ambayo ilihudhuliwa pia na viongozi wa juu wa dini hiyo mkoani hapa.
“Nitoe wito kwa wasanii wa Singida na nje ya Singida kuacha mara moja michezo ya kutafuta kiki za kuchezea alama za dini niwahusie wasanii wanawake wafanye usanii wao bila kujishubirisha na wanaume wala na mavazi yao na halikadharika na wasanii wa Wanaume waache kujishahibisha na wanawake na walakuvaa nguo zao” alisema Sheikh Nassoro.
Sheikh Nassoro alisema iwapo kutakuwa na ujumbe ambao unatakiwa kufikishwa kwa wanawake inapaswa watafutwe wao na si watafutwe wanaume na kuwa na hata kwa wanaume iwe hivyo hivyo na kujimithirisha kuwa mwanamke jambo ambalo halikubaliki hata kidogo.
Alisema hivi sasa tupo katika mapambano ya kupinga vitendo vya ubaradhuri (ushoga) lakini tutafanikiwaje kushinda mapambano hayo wakati wanaona kuna wanaume wanajimithirisha na jambo hilo na kwamba hawakubaliani na vitendo hivyo na wameiomba Serikali kuliangalia kwa karibu.
Alisema waislam wanalaani sana kitendo kilichoonekana hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii wanawake wakionekana
wakitangaza biashara huku wakiwa wamevaa kanzu za kiislam kuwa hawakubaliani na jambo hilo wao wanahesabu kama ni chokochoko dhidi ya waislam na kuwa wanaiambia Serikali kuwa mwanzo wa uvunjifu wa amani hapa nchini ni masuala madogomadogo kama hayo.
Sheikh Nassoro alisema wakati vitendo hivyo vikitokea wameibuka baadhi ya wanasheria wakiwemo waislam ambao wanatetea vitendo hivyo wakieleza kuwa eti wanao vifanya wana haki ya kufanya hivyo na watahakikisha wanawatetea kuipata hivyo aliwahimiza waislam kkujitokeza kumuunga mkono Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry Bin Ali kwenye maandamano ya kupinga vitendo hivyo yatakayo fanyika kuanzia Msikiti wa Masjid Taqwa hadi Stendi ya Zamani.
Mbunge wa Singida mjini Musa Sima alisema ujumbe mzito alioutoa Sheikh Nassoro wa kupinga vitendo hivyo unapaswa kuungwa mkono na kuomba Aprili 16, 2023 siku iliyopangwa kufanyika maandamano ya kupinga vitendo hivyo hapa Singida wananchi wajitokeze kwa wingi.
Aidha, Mbunge Sima alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na Mkoa wa Singina ukiwa ni mnufaika wa fedha hizo.
Mbunge Sima aliwaomba waislam kutumia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na hata baada ya mwezi huo kuendelea kutenda mema ili Mkoa wa Singida uwe mfano kwa
mikoa mingine.
Sima aliwaomba wananchi wa Mkoa wa Singida na mikoa mingine kumuombea kwa Mungu Rais Samia ili awe na afya na maisha marefu na kuendelea kuwaongoza watanzania.
Sheikh Nassoro akizungumza na wa umini wa kiislam wakati wa dua hiyo ya kumuombea baba yake.
Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro akiwa na Mbunge wa Singida Mjini baada ya futari iliyoandaliwa na Sheikh huyo nyumbani kwa baba yake Majengo mjini hapa na kuhudhuliwa na mamia ya waislam mkoani hapa.
Vijana wa kiislam wakionesha umahiri wa kuzikiri wakati wa dua hiyo.
Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro (kulia) akiwa na viongozi wengine wakati wa dua hiyo.