Na: Mwandishi wetu.
UONGOZI wa Simba umethibitisha kuachana na Hitimana Thiery ambaye alikuwa kocha msaidizi wa timu yao.
Awali ilikuwa ni tetesi kwamba huenda Simba ikampa mkono wa kwa heri kocha huyo ambaye alikuja kuchukua majukumu ya Didier Gomes kwenye mashindano ya CAF.
Kwa sasa Simba ipo chini ya Kocha Mkuu Pablo ambaye huyu ana vigezo vinavyotakiwa na CAF hivyo anakaa kwenye benchi katika mechi za mashindano tofauti na Gomes ambaye alikuwa anakaa jukwaani.
Taarifa rasmi kutoka kwenye dawati la Habari la Simba iliyotolewa leo Desemba 28 imeeleza kuwa :”Uongozi wa Klabu ya Simba umefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Msaidizi Hitimana Thiery, kuanzia leo Desemba 28,2021.
“Simba inamshukuru Hitimana kwa mchango wake aliotoa kwa timu tangu alipojiunga nasi tunamtakia kila la kheri katika maisha yake popote aendako,” ilieleza taarifa hiyo.