Home SPORTS SIMBA SC YAACHANA NA HITIMANA

SIMBA SC YAACHANA NA HITIMANA


Na: Mwandishi wetu.

UONGOZI  wa Simba umethibitisha kuachana na Hitimana Thiery ambaye alikuwa kocha msaidizi wa timu yao.

Awali ilikuwa ni tetesi kwamba huenda Simba ikampa mkono wa kwa heri kocha huyo ambaye alikuja kuchukua majukumu ya Didier Gomes kwenye mashindano ya CAF.

Kwa sasa Simba ipo chini ya Kocha Mkuu Pablo ambaye huyu ana vigezo vinavyotakiwa na CAF hivyo anakaa kwenye benchi katika mechi za mashindano tofauti na Gomes ambaye alikuwa anakaa jukwaani.

Taarifa rasmi kutoka kwenye dawati la Habari la Simba iliyotolewa leo Desemba 28 imeeleza kuwa :”Uongozi wa Klabu ya Simba umefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Msaidizi Hitimana Thiery, kuanzia leo Desemba 28,2021.

“Simba inamshukuru Hitimana kwa mchango wake aliotoa kwa timu tangu alipojiunga nasi tunamtakia kila la kheri katika maisha yake popote aendako,” ilieleza taarifa hiyo.

Previous articleMHE. HAMAD HASSAN CHANDE AFANYA ZIARA YA KIKAZI TEA
Next articleFURSA ZA UWEKEZAJI TANZANIA ZAENDELEA KUNADIWA KWENYE MAONESHO YA EXPO DUBAI 2021
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here