Home SPORTS YANGA, SIMBA ZAANZA VIZURI MAPINDUZI CUP

YANGA, SIMBA ZAANZA VIZURI MAPINDUZI CUP

 

SIMBA YAPETA MAPINDUZI CUP HUKU YANGA SC IKIENDELEZA UBABE, NKANE AONESHA BALAA LAKE

SayariJanuary 05, 2022


 ZANZIBAR

Leo mechi mechi mbili zimechezwa katika michuano ya Mapinduzi Cup ambapo Simba Sc iliingia uwanjani jioni ya leo kuvaana na timu ya Selem View na kufanikiwa kuondoka na Ushindi wa mabao 2-0.

Mabao ya Simba Sc yaliwekwa kimyani na nyota wao Pape Sakho akiifunga dakika ya 25 ya mchezo kipindi cha kwanza, na bao la pili likifungwa na kiungo wao Bwalya dakika ya 53 ya mchezo.

Katika mechi nyingine iliyopigwa usiku huu ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo Yanga wakimenyana na timu ya Taifa ya Jang’ombe na kufanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 2-0.

Mabao ya Yanga yalifungwa na na mshambuliaji wao Ebenezer Makambo pamoja na nyota mpya waliomsajili hivi karibuni Denis Nkane.
Previous articleMATOLA AWAMWAGIA PONGEZI WACHEZAJI KWA USHINDI WA BAO 2-0
Next articleKUTOKA MEZA YA MAGAZETI ASUBUHI YA LEO JANUARI 6-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here