Home SPORTS MATOLA AWAMWAGIA PONGEZI WACHEZAJI KWA USHINDI WA BAO 2-0

MATOLA AWAMWAGIA PONGEZI WACHEZAJI KWA USHINDI WA BAO 2-0


ZANZIBAR.

KOCHA  msaidizi wa Simba Seleman  Matola amesema kuwa ushindi ambao wameupata leo ni furaha kwao na pongezi kwa wachezaji.
Ushindi wa mabao 2-0 dhidi Selem View ambao walikwama kupiga shuti ambalo limelenga lango mbele ya Simba.
Ni mabao ya Pape Sakho dakika ya 24 na liliweza kudumu mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili Simba walipachika bao dakika ya 53 na kuwafanya Simba kuondoka na ushindi katika kundi C na wanakibarua cha kusaka ushindi katika mchezo wao ujao dhidi ya Mlandege.
“Furaha kwetu kupata pointi tatu na pongezi kwa wachezaji namna ambavyo wameweza kufanya hivyo kazi bado inaendelea,”.
Kwenye mchezo wa leo Rally Bwalya amechaguliwa kuwa mchezaji bora na amesepa na zawadi ya shilingi laki tano

Previous articleMAKAMU WA RAIS DKT.MPANGO ATEMBELEA BONDE LA MUZAKWE
Next articleYANGA, SIMBA ZAANZA VIZURI MAPINDUZI CUP
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here