Timu ya Taifa ya Cameroon wameanza vyema Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kutoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Burkina Faso katika mchezo wa Kundi A jioni ya leo Uwanja wa Paul Biya Jijini Yaounde.
Mabao yote ya Cameroon yamefungwa na mshambuliaji wa Al Nassr ya Saudi Arabia, Vincent Aboubakar kwa penalti dakika ya 40 na 45 baada ya Burkina Faso kutangulia kwa bao Gustavo Sangare dakika ya 25