Home LOCAL TANZANIA YAPOKEA MSAADA WA DAWA, VIFAA TIBA KUTOKA NCHINI MISRI

TANZANIA YAPOKEA MSAADA WA DAWA, VIFAA TIBA KUTOKA NCHINI MISRI


Na. Wizara ya Afya – Dar es Salaam
 
Serikali kupitia Wizara ya Afya imepokea msaada wa dawa pamoja na vifaa tiba vyenye thamani ya Tsh: Mil. 864 vitavyosaidia katika kupambana dhidi ya magonjwa mbalimbali kutoka katika Serikali ya Misri. 

Msaada huo umetolewa katika  uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam kupitia kwa Balozi Misri  nchini Tanzania Mhe. Mohamed Gaber Abouelwafa na kupokelewa na katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi kwa niaba ya Mhe. Ummy  Mwalimu, Waziri wa Afya.

Akipokea msaada huo, Prof. Makubi amesema, msaada huo umeletwa baada ya ziara ya kikazi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kutembelea nchini Misri mnamo mwezi November mwaka jana (2021).


“Tunamshukuru sana Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Tanzania pamoja na Serikali ya Misri kwa kushirikiana na Tanzania hasa katika kuboresha Sekta ya Afya kwa kusaidia mahitaji mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.” Amesema Prof. Makubi.

Aidha Prof. Makubi amesema msaada huo utaenda kuwasaidia wananchi wenye uhitaji katika  vituo mbali mbali vya kutolea huduma za afya nchini. 

Kwa upande wake Balozi wa Misri nchini Tanzania  Mohamed Gaber Abouelwafa amesema kujitoa kwa Serikali ya Misri, kusaidia Sekta ya Afya ni kutokana na jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo wananchi, ikiwemo kuboresha Sekta ya Afya nchini kwa kupambana dhidi ya magonjwa. 


“Serikali ya Misri itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kusaidia Maendeleo ya Watanzania, hasa katika kuboresha Sekta ya Afya, hii inatokana na nia njema ya Mhe. Rais Samia  katika kuleta maendeleo kwa wananchi, hususan katika kuboresha Sekta ya afya.” Amesema Mhe. Balozi Abouelwafa.

Kwa uongozi makini chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, Serikali ya Misri imetoa ahadi kuendelea kusaidi Sekta ya Afya nchini kwa kuendelea kuleta Dawa pamoja na vifaa tiba kwaajili ya kupambana dhidi ya Magonjwa mbalimbali. 

Mwisho.

Previous articleRANI YAENDELEA KUZINEEMESHA TIMU ZA WANAWAKE LIGI KUU
Next articleTUME YA MADINI YATOA BEI ELEKEZI KWA KWA BAADHI YA MADINI YANAYOZALISHWA NCHINI.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here