Home BUSINESS KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA MIRADI INAYORATIBIWA NA OFISI YA MAKAMU WA...

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA MIRADI INAYORATIBIWA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akifafanua jambo wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira ya kutembelea na kukagua shamba darasa la mahindi yaliyopandwa kwa kilimo cha kuhimili ukame katika Kijiji cha Sigili kupitia Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika Maeneo Kame nchini (LDSF) katika Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Mhe. Jackson Kiswaga akizungumza wakati wa ziara ya kamati hiyo ya kutembelea na kukagua ujenzi wa ghala la kuhifadhia mazao na eneo la kusimika mashine ya kukoboa mpunga katika Kijiji cha Bulambuka unaotekelezwa kupitia Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika Maeneo Kame nchini (LDSF) katika Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira wakiwa katika ziara ya kutembelea na kukagua shamba darasa la mahindi yaliyopandwa kwa kilimo cha kuhimili ukame katika Kijiji cha Sigili kupitia Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika Maeneo Kame nchini (LDSF) katika Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Mhe. Jackson Kiswaga akipanda mti katika Kijiji cha Sigili wakati wa ziara ya kamati hiyo ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika Maeneo Kame nchini (LDSF) katika Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo.
Jengo la ghala la kuhifadhia mazao na eneo la kusimika mashine ya kukoboa mpunga katika Kijiji cha Bulambuka likiwa katika hatua za ujenzi wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika Maeneo Kame nchini (LDSF) katika Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Jengo la kukusanyia mazao ya nyuki katika Kijiji cha Sigili likiwa katika hatua za ujenzi wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika Maeneo Kame nchini (LDSF) katika Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira imeonesha kuridhishwa na utekelezaji wa Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika Maeneo Kame nchini (LDSF) katika Wilaya ya Nzega mkoani Tabora.

Hayo yamejiri leo Machi 16, 2023 wakati wa ziara ya kamati hiyo ya kukagua ujenzi wa jengo la kukusanyia mazao ya nyuki, banda la kuku, shamba darasa na uchimbaji wa visima chini ya mradi huo unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.

Akizungumza wakati wa ziara Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Jackson Kiswaga amepongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa usimamizi na ufuatiliaji wa mradi huo akisema umelinana na thamani ya fedha zilizotolewa.

Mhe. Kiswaga amesema kuwa mradi wa ufugaji wa nyuki katika Kijiji cha Sigili wlayani hapo ni wa mfano kwani unasaidia kuhifadhi na kulinda mazingira kupitia misitu ambayo mizinga imetundikwa.

Hivyo, ametoa wito kwa wananchi kuendelea kupanda miti na kuitunza ili kuweza kukabiliana na athari hasa za kimazingira ambazo zinasababisha ukosefu wa mvu katika maeneo mbalimbali nchini.

“Ndugu zangu sisi Bunge kama Chombo kinachosimamia maendeleo ya wananchi tumejifunza mambo makubwa hapa Nzega kwenye mradi huu na tutautumia kama mfano kuwaelemisha katika maeneo mengine ili nao wajifunze,“ amesema Mhe.Kiswaga.

Wajumbe wa kamati hiyo pamoja na kutoa pongezi pia wametoa ushauri kuwa miradi kama hiyo itekelezwe katika maeneo mengine ya nchi wananchi wanufaike nayo.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira kwa kutembelea mradi huo na kuona namna Serikali inavyohakikisha wananchi wake wananufaika na miradi ya mazingira.

Pia, ameahidi kuwa Ofisi itaendelea kuisimamia vyema miradi hii ili iendelee kuleta matokeo mazuri kwa wananchi hasa katika eneo la kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi linalolikabili taifa letu.

“Niwapongeze Halmashauri ya Nzega kupitia kwa Mkurugenzi wake na wataalamu wote kwa kufanya vizuri katika mradi huu na sisi kama Ofisi ya Makamu wa Rais tutahakikisha tunausimamia vizuri mradi huu,“ amesema.

Mradi wa LDFS unafadhiliwa na Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF) na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) na kuratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais ambapo unatekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega (Tabora), Magu (Mwanza), Mkalama (Singida), Kondoa (Dodoma) na Micheweni (Pemba).

Previous articleWAKANDARASI WALIOGOMEA WITO WA DKT. MOLLEL WA KUFIKA ENEO LA KAZI WAELEKEZWA KUFIKA KWA MKUU WA MKOA
Next articleGGML INAIBEBA GEITA , WIZARA YA MADINI KUTAFSIRI VEMA MABORESHO SHERIA YA MADINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here