Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akimkabidhi Tuzo mshindi wa kwanza aliyefanya vizuri katika kuzalisha Bidhaa za Kiasili katika hafla iliyoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC) Machi 11,2023 katika Ukumbi wa Mlimani city Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akizungumza katika hafla hiyo muda mfupi kabla ya kuanza zoezi wa utoaji wa Tuzo za Bidhaa za Viwanda Wanawake Wajasiriamali Jijini Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali na wageni walioakikwa kwenye hafla hiyo wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri Kigahe alipokuwa akizungumza Katika hafla hiyo
Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi Bi. Beng’i Issa akizungumza alipokuwa akitoa hotuba yake kumkaribisha Mgeni rasmi.
Mwenyekiti wa TWCC Taifa Bi. Mercy Silla akizungumza alipokuwa akitoa salamu za utangulizi na kuzielezea Tuzo hizo zinazotolewa na Taasisi hiyo Kila mwaka.
Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC Mwajuma hamza akizungumza alipokuwa akizielezea Tuzo hizo zinazotolewa na Taasisi hiyo kila mwaka.
Mkurugenzi Mtendaji wa GS1 Tanzania Fatma Kange (kushoto) akimkabidhi tuzo na Cheti moja ya mshindi katika hafla hiyo
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe mwenye (suti) akicheza muziki pamoja na viongozi na wanachama mbalimbali wa TWCC katika hafla hiyo.
(PICHA NA: HUGHES DUGILO)
Na: Hughes Dugilo, DAR
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Exaud Kigahe amesema kuwa Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa Wajasiriamali kupata fursa ya kuuza bidhaa zao ndani na nje ya nchi.
Mheshimiwa Kigahe ameyasema hayo Machi 11, 2023 katika hafla ya utoaji tuzo za Wanawake wanaozalisha bidhaa za Viwandani zilizoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC) iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani city Jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wakiwemo TWCC imekuwa ikitambua bidhaa zinazo zalishwa na Wajasiriamali hapa nchini na kwamba kwa kupitia majukwaa yao kumekuwa na fursa nyingi zinazolenga kuwasaidia Wajasiriamali hao kufikisha bidhaa zao kwenye masoko mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Aidha ameipongeza TWCC kwa jitihada kubwa wanazofanya katika kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kuwawezesha na kuwainua Wanawake wafanyabiashara kote nchini.
“Ni wazi kuwa Mwanamke akiwezeshwa katika Biashara uchumi wake utaimarika na kumili kipato chake ataweza kuisaidia familia yake na kukuza uchumi wa familia na Taifa kwa ujumla” amesema Mhe. Kigahe
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa TWCC Taifa Bi.Mercy Silla amesema kuwa Tuzo hizo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambapo kila mwaka TWCC inasherehekea siku hiyo kwa kuandaa maonesho ya Wajasiriamali kuonesha bidhaa zao wanazozalisha na kuhitimisha kwa hafla kubwa ya utoaji tuzo kwa Wajasiriamali wao.
Sherehe hizo za utoaji tuzo kwa Wajasiriamali ziliudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka Serikalini, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Taasisi za Umma, pamoja na Sekta Binafsi, ambapo jumla ya tuzo 70 zilitolewa.