Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Mhe. Ummy Mwalimu mapema leo Januari 25, 2022 ametembelea Zanzibar na kushuhudia teknolojia ya haraka ya kupima UVIKO-19 kwa kutumia akili bandia (Artificial Intelligence) vifaa vilivyofungwa uwanja wa Ndege wa Aman Abeid Karume.
Katika ziara hiyo, Waziri Ummy Mwalimu amekutana na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Nassor Mazrui na kubadilishana uzoefu kuhusu vipimo vya Corona pamoja na utoaji wa chanjo.
Waziri Nassor Mazrui alibainisha kuwa, Zanzibar imepiga hatua katika utoaji wa chanjo kwa wananchi ambapo umefikia asilimia 16 lakini lengo likiwa asilimia 60 ya Wazanzibar wote.
Waziri Ummy pia alipata kupata nafasi ya kutembelea eneo la kupima Covid-19 lililopo Migombani na Uwanja huo wa ndege wa Amani Abeid Karume ambao wameweka teknolojia ya haraka ya kupima UVIKO-19 kwa kutumia akili bandia (Artificial Intelligence) ndani ya sekunde moja mtu anaweza kubainika kama ana vimelea au hana .
Mwisho.