Home BUSINESS WATUMISHI WANAWAKE BRELA WAPONGEZWA KWA UCHAPAKAZI

WATUMISHI WANAWAKE BRELA WAPONGEZWA KWA UCHAPAKAZI

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Godfrey Nyaisa (katikati), akishirikiana na watumishi wa BRELA Bi. Yvone Masele(kushoto) na Bi.Anna Nderingo(kulia), kukata keki ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, katika ofisi za BRELA jijini Dar es Salaam leo.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Godfrey Nyaisa akiwalisha keki baadhi ya watumishi Wanawake WA Taasisi hiyo kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani Machi 8,2023.

Bi.Anna Nderingo mhasibu wa BRELA, akimlisha keki Afisa Mtendaji mkuu wa BRELA Bw.Godfrey Nyaisa ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani katika ofisi za BRELA.

Wanawake wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni wakiwa katika picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu Bw. Godfrey Nyaisa (katikati) kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mapema leo tarehe 8 machi, 2023 ofisi za BRELA Makao Makuu jijini Dar es Salaam.

DAR ES SALAAM 

Watumishi wanawake wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), wamepongezwa kwa utendaji kazi mzuri na kutakiwa kuendelea kuzingatia sheria na kanuni za kazi na kuiwezesha Taasisi kufikia malengo yake.

Pongezi hizo zimetolewa tarehe 8 Machi, 2023 na Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Bw. Godfrey Nyaisa, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku wa Wanawake Duniani, katika ofisi za BRELA jijini Dar es Salaam.

Bw. Nyaisa amewapongeza wanawake wa BRELA kwa kuendelea kutimimza majukumu yao kwa weledi wakati wote.

“Kwanza niwapongeze wanawake wote kwa pamoja pia muongeze bidiii katika kutimiza majukumu yenu ikiwa ni pamoja na kuzingatia Maadili Sheria na Kanuni za kazi” amesema Bw. Nyaisa.

“Wanawake mmekua chachu ya mafanikio makubwa, wengi wenu mnajitoa kwenye shughuli nyingi, mwanamke wa sasa sio kama wa kale, hivyo hongereni kwa kuwa mstari wa mbele kwenye kupambania maisha yenu na ninawatakia maadhimisho mema na maandamano yenye tija wanawake wote”, amesisitiza Bw. Nyaisa.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Miliki Ubunifu Bi. Loy Mhando, amewapongeza wanawake kwa kujituma na kujitambua kwenye kutimiza majukumu yao ya kila siku.

Aidha Bi. Mhando amewataka Wanawake wa BRELA kutokata tamaa mara wanapokumbana na changamoto zozote.

Wanawake wa BRELA baada ya kupata nasaha hizo walishiriki katika maandamano yaliyoandaliwa kimkoa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja na kisha kupeleka mahitaji muhimu kwa wagonjwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kituo cha kulea watoto yatima cha Maunga Center, kilichopo kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake huadhimishwa tarehe 8 Machi kila mwaka duniani kote.

Previous articleMAGAZETI YA LEO ALHAMISI MACHI 9,2023
Next articleBRELA YAWAJENGEA UWEZO WADAU KUHUSU KANUNI ZA WAMILIKI MANUFAA WA KAMPUNI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here