Home BUSINESS BRELA YAPIGA KAMBI YA SIKU TANO KUSIKILIZA, KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYABIASHARA JIJINI...

BRELA YAPIGA KAMBI YA SIKU TANO KUSIKILIZA, KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYABIASHARA JIJINI DAR

Afisa habari BRELA Bi. Sheila Mfunami (aliyevaa fulana nyeusi) akizungumza na wateja waliofika kwenye Banda lao kupata huduma za Taasisi hiyo Katika katika viwanja vya Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Afisa Tehama wa BRELA Joram Manyika (kulia) akizungumza na Justinianius Kampuni (kushoto), mteja aliefika katika Banda lao kwaajili ya kupata huduma.

Afisa Tehama wa BRELA Joram Manyika (kulia) akizungumza na Felister Ngoli (kulia) mteja aliefika katika Banda la Taasisi hiyo Katika katika viwanja vya Mlimani City Jijini Dar es Salaam kwaajili ya kupata huduma.

Afisa Leseni wa BRERA Sada Kilabula akizungumza na waandishi wa habari
Afisa Leseni wa BRERA Sada Kilabula akizungumza na waandishi wa habari akiwa na Afisa Usajili Ruth Mmbaga (kulia) katika viwanja vya Mlimani City Jijini Dar es Salaam leo. (PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO).

Na: Hughes Dugilo, DAR

Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na viunga vyake wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Mlimani City Jijini humo  ili kuweza kukutana na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni  (BRELA) ambao wameweka Kambi kwenye viwanja hivyo kusikiliza na kutatua changamoto zinazoikabili wafanyabiashara.

Afisa Leseni wa BRERA Sada Kilabula ameyasema hayo leo Januari 25,2022 wakati alipozungumza na waandishi wa habari ikiwa ni siku ya kwanza ya Kambi hiyo.

Amesema kuwa BRELA itakuwa hapo kwa siku tano kuanzia leo Januari 26 na kufikia tamati Januari 30 siku ya jumapili mwaka huu.

“BRELA tuko hapa kwa siku tano kusikiliza changamoto mbalimbali za wananchi na kuzipatia ufumbuzi na kuwasaidia kufanya usajili wa Biashara zao pia” Amesema Sada.

Aidha ameongeza kuwa katika Kambi hiyo watatoa fursa ya kuwasaidia wananchi  kufahamu jinsi ya kutumia mifumo ya kielektonic itakayowasaidia kupata taarifa mbalimbali za Wakala na kufanya usajili kwa njia ya mtandao.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliofika viwanjani hapo kupata huduma wameishukuru BRELA kuwasogezea huduma na kwamba itawasaidia kupata taarifa sahihi na kupata huduma zote kwa wakati mmoja.

“Uwepo wa BRELA hapa kumenipa fursa ya kufanikisha kurekebisha taarifa za  Kampuni yetu, imetusaidia sana kwani imetuokolea muda na imerahisisha sana” Ameeleza Frank Mambali.

Nae Mjasiriamali Marco Luwena ameipongeza BRELA kwa ubunifu mkubwa walioufanya wa kusogeza huduma zao kwa wananchi na kutoa wito kwa wananchi kuitumia vema fursa hiyo.

“Kwakweli huu ni ubunifu mkubwa sana tunapaswa kuwapongeza na kuwashukuru sana BRELA kutupa fursa hii” Amesema Marco.

Uwepo wa Kambi hiyo ya siku tano inatoa  fursa kwa BRELA kutekeleza majukumu yake kwa wananchi yakiwemo, Usajili wa Makampuni, Usajili wa Majina ya Biashara, Usajili wa Alama za Biashara na Huduma, Utoaji wa hataza, Utoaji wa Leseni za Viwanda, Huduma za Baada ya Usajili na kupata Leseni, na Huduma za kupata taarifa kwa Mtandao.

Mwisho. 


Previous articleMAHAKAMA KUU KANDA YA SONGEA YATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA MFARANYAKI
Next articleYASEMAVYO MAGAZETI ASUBUHI YA LEO ALHAMISI JANUARI 27-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here