Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ameshiriki mkutano wa 150 wa bodi tendaji ya Shirika la Afya duniani ulioanza Januari 24 na kumalizika kesho Januari 29 2022 kwa njia ya mtandao huku washiriki wengine wakiwa Wizara ya Afya kutoka Tanzania bara na Visiwani , Ofisi ya Rais TAMISEMI, pamoja na maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uswisi.
Tanzania imewasilisha jumla ya maandiko 9 katika ajenda 8 za mkutano huu huku maeneo yaliyoandaliwa ni afya ya mama, mtoto na lishe,
Magonjwa yasiyoambukiza, kifua kikuu, UKIMWI, magonjwa ya via vya uzazi na ngono, homa ya Ini, mafua makali ya influenza, polio na chanjo.
Waziri Ummy aliwasilisha andiko la afya ya kinywa na meno ambapo alitoa mwelekeo na mikakati ambayo Tanzania imejiwekea kuimarisha huduma katika eneo hilo.
Aidha, maandiko mengine yaliwasilishwa na wataalam mbalimbali waliohudhuria mkutano huo.