Home LOCAL WAZIRI UMMY ASHIRIKI MKUTANO WA 150 WA BODI TENDAJI YA WHO

WAZIRI UMMY ASHIRIKI MKUTANO WA 150 WA BODI TENDAJI YA WHO

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ameshiriki mkutano wa 150 wa bodi tendaji ya Shirika la Afya duniani ulioanza Januari 24 na kumalizika  kesho Januari 29 2022 kwa njia ya mtandao huku washiriki wengine wakiwa Wizara ya Afya kutoka  Tanzania bara na Visiwani , Ofisi ya Rais TAMISEMI, pamoja na maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uswisi.

Tanzania imewasilisha jumla ya maandiko 9 katika  ajenda 8 za mkutano huu huku maeneo yaliyoandaliwa ni afya ya mama, mtoto na lishe, 

Magonjwa yasiyoambukiza, kifua kikuu, UKIMWI, magonjwa ya via vya uzazi na ngono, homa ya Ini, mafua makali ya influenza, polio na chanjo.

Waziri Ummy aliwasilisha andiko la afya ya kinywa na meno ambapo alitoa mwelekeo na mikakati ambayo Tanzania imejiwekea kuimarisha huduma katika eneo hilo.

Aidha, maandiko mengine yaliwasilishwa na wataalam mbalimbali waliohudhuria mkutano huo.

Previous articleMGANGA MKUU WA SERIKALI DKT. SICHALWE ATAKA KASI YA HAMASA KWA WANANCHI KIGOMA ILI KUPATA CHANJO YA UVIKO 19
Next articleMOTO WAUNGUZA MADUKA 16 SOKO LA CCM KAKUBILO GEITA.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here