Home LOCAL RC MAKALLA AFURAHISHWA NA MWITIKIO MZURI WA WANANCHI KUSHIRIKI KATIKA ZOEZI...

RC MAKALLA AFURAHISHWA NA MWITIKIO MZURI WA WANANCHI KUSHIRIKI KATIKA ZOEZI LA USAFI WA PAMOJA

Ashiriki zoezi la Usafi wa pamoja Manzese.

– Asema Mpango wa Serikali kwa Wafanyabiashara ni kuwapanga vizuri, kusafisha, kuboresha maeneo waliyopangwa na kuhakikisha hawarudi kwenye maeneo yaliyokatazwa.

– Awaeleza kuwa Vitambulisho vya Machinga na Fursa ya mikopo itatolewa kwa wale Wanaofanya biashara kwenye maeneo rasmi pekee.

Na: James Lyatuu, DAR ES SALAAM.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo ameshiriki zoezi la Usafi wa pamoja kata ya Manzese ambapo ametumia Fursa hiyo kuwaeleza Wafanyabiashara kuwa zoezi la utoaji wa Vitambulisho vya Machinga na Fursa ya mikopo itatolewa kwa wale Wanaofanya biashara kwenye maeneo rasmi pekee.

RC Makalla amesema hayo wakati wa zoezi la Usafi ikiwa ni sehemu ya Kampeni ya Safisha, Pendezesha Dar es salaam ambapo kila Jumamos ya mwisho wa Mwezi imepangwa kuwa siku ya Usafi wa pamoja.

Aidha RC Makalla amesema Mpango wa Serikali kwa Wafanyabiashara Ni kuwapanga vizuri, kusafisha maeneo, kuboresha maeneo walipopelekwa na kuyalinda maeneo waliyohama ili yasivamiwe upya.

Hata hivyo RC Makalla amesema Hali ya Usafi kwa Jiji hilo kwa Sasa inaridhisha Kutokana na Wananchi kuona umuhimu wa kufanya Usafi na kutoa wito kwa Wananchi kuendelea kusafisha maeneo yao.

Zoezi la Usafi wa pamoja Wilaya ya Ubungo eneo la Manzese limehudhuriwa pia na Viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya, Mstahiki Meya, Madiwani, Wakuu wa idara, wenyeviti wa Mitaa Na Wananchi.

Previous articleKARIBU USOME MAGAZETI YA LEO J.MOSI JANUARI 29,2022
Next articleNAIBU WAZIRI MARY MASANJA AZINDUA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA UVIKO 19 KWA WATOA HUDUMA ZA UTALII DAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here