Home LOCAL WATU WANAOKUTWA NA UTI MARA KWA MARA WANAWEZA KUWA NA MAWE KWENYE...

WATU WANAOKUTWA NA UTI MARA KWA MARA WANAWEZA KUWA NA MAWE KWENYE FIGO

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya mfumo wa mkojo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt Remigius Rugakingira,  ameshauri watu wanaokutwa na UTI mara kwa mara wafanye uchunguzi wa kina kwani wanaweza kuwa na mawe kwenye figo.

Dkt Rugakingira amesema kuna baadhi ya bakteria kwenye mfumo wa mkojo ambao wanafanya utengenezaji wa mawe kuwa mkubwa.

“Mtu anayetibiwaa UTI mara kwa mara anaweza kuwa na bakteria wengi ambao wanatengeza mawe kwenye figo kwa hiyo, ni bora akafanya uchunguzi wa kina” alisema Daktari.

Alifafanua kuwa Hospitali ya Benjamin Mkapa wanaweza kuyabaini mawe hayo kupitia teknolojia ya vipimo ikiwemo CT SCAN na Utrasound na kuwa wanaweza kutibu tatizo hilo pasipo upasuaji kwa kuwa wana mashine ya Shock Wave Lithotripsy (SWL)

SWL ni mashine inayotumia teknolojia kuyeyusha au kuyaponda mawe na kuyatoa kwa njia ya mkojo.

Previous articleKAMATI YA SERA YA FEDHA YA BENKI KUU YARIDHISHWA NA MWENENDO MZURI WA UCHUMI
Next articleMSANII NAGWA KUACHIA NGOMA MPYA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here