Home LOCAL NIMEFURAHISHWA NA MIRADI YA KIMAENDELEO-MAJALIWA

NIMEFURAHISHWA NA MIRADI YA KIMAENDELEO-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema anafurahishwa na mafanikio makubwa ya utekelezwaji wa ujenzi miradi mbalimbali ya maendeleo yanayoonekana katika maeneo mbalimbali nchini yakiwemo ya wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

“Wana-Ruangwa lazima tuendelee kumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuidhinisha fedha nyingi za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Haya ni mafanikio makubwa, Ruangwa kwa maendeleo inawezekana.”

Amesema hayo leo (Jumatano, Februari 22, 2022) baada ya kukagua ujenzi wa jengo la utawala shule ya Sekondari ya Wasichana Ruangwa (Ruangwa Girls) pamoja na madarasa katika Shule ya Sekondari ya Kitandi wilayani Ruangwa.

Mheshimiwa Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia anaridhia kutoa fedha kwa ajili ya kujenga miundombinu mbalimbali ya utoaji huduma za jamii hapa nchini hivyo ni jukumu la kila wananchi ni kuitunza ili ilete faida anayoikusudia

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wanafunzi kwamba wajitahidi kufanya vizuri kwenye masomo yao “Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ameweka mkazo katika elimu, ambayo inatolewa bure kuanzia awali hadi kidato cha sita”

“Jitahidini kufanya vizuri kitaaluma, mjitambue nyie ni wanafunzi na hivyo mjiepushe na vishawishi vyovyote vitakavyokwamisha maendeleo yenu kitaaluma. Wananchi tuwalinde watoto wetu ili watimize ndoto zao. Mtoto wa mwenzio ni wako.”

Pia, Waziri Mkuu amewataka wananchi kuacha kuvamia maeneo ya karibu kwa kuwa Serikali imeyahifadhi kwa ajili matumizi ya baadae ya taasisi husika. “Hapa palikuwa pori hapakuwa na shamba pasiguswe.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amekagua ujenzi wa madarasa ya ghorofa yanayojengwa katika shule ya msingi Likangara, ambapo ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa kwa ubunifu wa mradi huo. Mradi huo unahusisha vyumba vinane vya madarasa, matundu 24 ya vyoo na ofisini nne.

Previous articleBENKI YA CRDB YAWAPA UBALOZI WACHEZAJI WA SIMBA NA YANGA KAMPENI YA YA BENKI NI SIMBANKING
Next articleMAGAZETI YA LEO ALHAMISI FEBRUARI 23 – 2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here