Home BUSINESS CBE YATAMBULISHA MITAALA INAYOKWENDA NA WAKATI 

CBE YATAMBULISHA MITAALA INAYOKWENDA NA WAKATI 

Kaimu Mkuu wa chuo hicho, Prof. Edda Tandi Lwoga, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kozi ambazo zitaanza kufundishwa mwezi  tisa Kushoto ni Mhadhiri Mwandamizi wa chuo hicho, Dk. Nasibu Mramba na kulia ni Mkuu wa Uhusiano wa chuo hicho, Leonidas Tibanga.

·  Yaja na kozi mpya lukuki

Na:  Mwandishi Wetu

CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimesema mpango wa kuwasaidia wanafunzi wajasiriamali kuendeleza biashara zao au kuatamia mawazo ya biashara zao utakuwa wa manufaa makubwa.

Chuo kimesema lengo la kufanya hivyo ni kutatua tatizo kubwa la ajira lililopo nchini kwa  kuwafanya wahitimu wa chuo hicho waendane na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia katika nyanja za biashara na uchumi.

Hayo yalisemwa jana na  Kaimu Mkuu wa chuo hicho, Prof. Edda Tandi Lwoga, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kozi ambazo zitaanza kufundishwa mwezi  tisa.

Alitaja baadhi ya kozi hizo kuwa ni Astashahada ya Msingi ya Uchumi na Fedha, Astashahada ya Msingi ya Usimamizi wa Usafirishaji, Astashahada ya Msingi ya Ujasiriamali na Ubunifu,  Astashahada ya Msingi ya Uongozi wa Biashara, Usimamizi wa Kumbukumbu na Makavazi, Astashahada ya msingi ya Digital Marketing na Astashahada ya Msingi ya Masoko na Utalii .

“Katika ngazi hii tunampokea mwanafunzi ambaye amemaliza kidato cha nne na kufaulu walau masomo manne. Hapa tunaanza kumpa elimu ya Msingi katika fani husika,” alisema.

Alisema kasi inayoongezeka kila mara ya mabadiliko ya kiteknolojia katika nyanja za biashara na uchumi yamekuwa chachu kwa Chuo kuwaandaa wahitimu wanaoendana na mabadiliko hayo.

“CBE imejielekeza zaidi kusaidia katika kutoa mafunzo kwa wahitimu wenye ujuzi wa biashara kwa uchumi wa Tanzania. Chuo kinatambua kuwa maendeleo ya rasilimali watu wenye ujuzi kwa uwezeshaji wavijana, tija, na ufanisi katika jamii unategemea wakufunzi wenye ujuzi na uzoefu, na ubora wa taasisi za mafunzo,” alisema.

Profesa Tandi alisema Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kwa miaka 58 sasa kimekuwa kikitoa huduma bora katika jamii kwa kutoa elimu ya biashara kwa wajasiriamali, kutoa wahitimu wenye ujuzi kulingana na uhitaji wa soko na kutoa mafunzo na kutoa ushauri wa kitaalamu.

Alisema mambo hayo yamejikita kwenye majukumu ya msingi ya Chuo ambayo ni Kutoa Taaluma, Kufanya tafiti na Kutoa Ushauri wa Kitaalamu. Ili kuwafikia wananchi wengi

Chuo kimeweka huduma hizi katika Kampasi zetu za Dar es salaam, Dodoma, Mwanza na Mbeya,” alisema .

Profesa Tandi alisema ili kutoa mchango kwenye Maendeleo ya Viwanda na Biashara Katika Ukuaji wa Uchumi Endelevu Tanzania, Chuo kimekuwa kinabadili mitaala yake na kuongeza kozi mpya zinazoendana na kuendeleza Uchumi, Biashara na Maendeleo ya viwanda.

Alisema katika kukabiliana na Mfumo wa Elimu ya Juu na Kutoa Wahitimu Wasio na Ajira

Tanzania, Chuo cha Elimu ya Biashara kimekuwa kikizidi kuongeza matarajio mengi kwa wahitimu kwa kuwapatia ujuzi unaohitajika na soko la ajira ikiwa ni pamoja na wahitimu wengi kuweza kujitegemea kwa kujiajiri.

“Chuo kimekuwa kikijitahidi kubadili mitaala, kubuni kozi mpya ikiwa ni pamoja na kutumia mbinu za kisasa za kufundishia.

Pia, Chuo kimeanzisha mafunzo ya Uanagenzi vilevile baadhi ya wanachuo kuwa

kwenye Atamizi za biashara.  Mafunzo ya uanagenzi yana msingi wa mafunzo kwa vitendo kwa kushirikiana na mahali halisi pa kazi. Hapa mwanachuo hutumia nusu ya muda

wake Chuoni na nusu kwa mwajiri ambapo hupata fursa ya kujifunza kwa vitendo mambo ambayo tayari amekwisha jifunza kwa nadhalia,” alisema

Mwisho.

Previous articleRAIS SAMIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA MHE. DKT. ABIY AHMED, JIJINI  ADDIS ABABA
Next articleUWT ILALA YAWATAKA WANAWAKE KUKAGUA VITABU NA MABEGI YA SHULE YA WATOTO WAO.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here