Home LOCAL RAIS SAMIA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA 26 YA GRIDI IMARA YENYE THAMANI...

RAIS SAMIA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA 26 YA GRIDI IMARA YENYE THAMANI YA SHILINGI TRILLION 1.9 IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akishuhudia Mkurugenzi wa Shirika la Umeme nchini TANESCO Maharage Chande akiwa pamoja na Mwanasheria wa Shirika hilo Zaharani Kisilwa wakati wakitia saini Mikataba mbalimbali ya Gridi Imara na Wakandarasi mbalimbali kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akishuhudia Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Umeme Vijijini REA Eng. Hassan Saidy pamoja na Mwanasheria wa REA Mussa Muze wakati wakitia saini Mikataba ya kupeleka Umeme maeneo mbalimbali nchini kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akishuhudia makabidhiano ya Hati baada ya kukamilika utiaji saini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa Mikataba 26 ya Gridi Imara yenye thamani ya Shilingi Trillion 1.9. Hafla ya utiaji saini Mikataba ya kuimarisha Gridi ya Taifa na usambazaji wa umeme Vijijini imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni mbalimbali mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa Mikataba 26 ya Gridi Imara yenye thamani ya Shilingi Trillion 1.9, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Previous articleMAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA KAHAWA CHA GDM MKONI SONGWE – 2
Next articleAMCOS MBOZI KUCHUNGUZWA-MAJALIWA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here