BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Twaha Kiduku amesaini mkataba wa kupanda ulingoni kuzichapa dhidi ya Alex Kabangu kutoka DR Congo katika pambano litakalopigwa Machi 26, mwaka huu Mkoani Morogoro.
Kiduku atapanda ulingoni kwenye pambano hilo la Kimataifa dhidi ya Kabangu baada ya kumchakaza Dullah Mbabe mwezi Agosti mwaka jana kwenye pambano la Usiku wa Deni lililopigwa Ubungo Plaza, Dar es salaam
Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo Kiduku amesema sapoti anayopewa na watanzania inazidi kumpa uwezo wa kufanya vizuri katika kila pambano huku akiahidi kuiandika historia kwa Mara nyingine kwa kumchakaza Vibaya Alex Kabangu.
“Ni kweli nimesaini kucheza pambano hilo ambalo litakuwa la mkanda wa ubingwa, naamini mkanda utabakia kwa sababu lazima nifanye maandalizi ya kutosha chini ya kocha wangu Pawa Ilanda na nguvu kubwa ninayo pewa na mashabiki zangu kwanza wa Morogoro na Watanzania Wote kwa Ujumla ambao hawajawahi kuniacha Tangu siku ya kwanza”
“Kila kitu tayari kimeshapangwa na promota juu ya siku ya pambano lakini maombi yangu ni kuweza kuwezasha pambano kufanyika mjini ili watu wengi waweze kuhudhuria taofauti na Magadu kwa sababu ni mbali na mjini.
Aidha Mratibu Mkuu kutoka Peaktime Media Meja Selemani Semunyu amesema pambano hilo la kimataifa litasindikizwa na Mabondia Nyota wa Morogoro akiwemo Joseph Mchapeni Dhidi ya Ally Mwerangi, Juma misari dhidi ya kareem Mandonga, Ayubu Mwankina na Wengine Wengi.
Mwisho.