Home SPORTS MORRISON AREJESHWA KIKOSINI

MORRISON AREJESHWA KIKOSINI

 

[2/15, 11:35 PM] Stella Journalist: Morrison arejeshwa kikosini Na: Stella Kessy

UONGOZI wa klabu ya Simba umemsamehe nakumrudisha kikosini Kiungo Mshambuliaji wao Bernard Morrison, baada ya kuomba radhi kwa makosa ya utovu wa nidhamu aliyoyafanya.

Morrison alisimamishwa kazi Februari 04 Mwaka huu kutokana na kutoroka kambini hivyo uongozi ulimtaka kwenda kujieleza kwenye ofisi ya mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Barbara Gonzalez na ndio amepata msamaha.

Akizungumza na Gazeti hili, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Simba SC, Ahmed Ally  aliweka wazi kuwa mchezaji huyo amesamehewa na atarejea kikosini kujiunga na wachezaji wenzake kujiandaa na michezo inayoikabili timu yao.

Morrison atakuwa sehemu ya kikosi cha Simba SC ambacho wiki hii kitasafiri kwenda kucheza mchezo wa pili wa hatua ya makundi nchini Niger, kisha wataunganisha Morocco kuwafuata RS Berkane.

“Bernard Morrison amesamehewa na atajinga nakikosi kwaajili ya maandalizi ya michezo tuliyonayo kama kawaida,” alisema.

Previous articleKIDUKU KUZICHAPA MWEZI UJAO
Next articleKOCHA PABLO AJIPANGA KIVINGINE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here