Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwanasiasa ambaye pia ni mmoja wa Viongozi Wakuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Antiphas Lissu leo tarehe 16 Februari, 2022 katika Jiji la Brussels nchini Ubelgiji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwanasiasa ambaye pia ni mmoja wa Viongozi Wakuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Antiphas Li leo tarehe 16 Februari, 2022 katika Jiji la Brussels nchini Ubelgiji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo mafupi na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Tundu Lissu Jijini Brussels nchini Ubelgiji leo Jumatano Februari 16,2022.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Zuhura Yunus, amesema Mazungumzo hayo yamefanyika baada ya Rais Samia kukubali maombi ya kiongozi huyo wa Chadema kukutana naye na kuzungumza jijini Brussels.
Aidha katika mazungumzo hayo Mhe. Rais na Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, walizungumza masuala mbalimbali yenye maslahi na ustawi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais Samia yupo nchini Ubelgiji kwa ziara ya kikazi aliyoianza jana.