NA: HERI SHAABAN (ILALA)
MWENYEKITI wa chama cha Mapinduzi (CCM )Mkoa Dar es Salaam Abas Mtemvu, ametoa BARAKA mchakato wa Kugawanya majimbo na Kata na mitaa Wilayani Ilala Ili Wananchi waweze kupata huduma za kijamii karibu na Makazi yao.
.Mwenyekiti Abas Mtemvu ametoa tamko hilo kata ya Zingiziwa Wilayani Ilala wakati Diwani wa Zingiziwa Maige Maganga alipowakuwa akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya mwaka 2020 mpaka 2023 .
“.Naomba nipewe maelekezo zile Kata kubwa ,Majimbo na Mitaa kwa ajili ya Kugawanya ,yatagawanywa naomba Madiwani na Viongozi wa chama mlete mapendekezo yenu tutafanya na vikao” alisema Mtemvu .
Mwenyekiti Mtemvu alisema amepokea changamoto ya Jimbo la Ukonga baadhi ya Kata kubwa zina mitaa minane hivyo kupelekea changamoto ya Shughuli za Kijamii na chama kutokana na umbali wake na kufika ina kuwa shida.
Mtemvu alisema baadhi ya changamoto alizopokea kero ya ukubwa katika Jimbo la Ukonga ,Kata za Msongola kubwa Kata Zingiziwa Majohe na Kata zingine zote ameomba apokee mapendekezo ya vikao
Mwenyekiti wa CCM kata ya Zingiziwa Abirah Mpate amemshauri Kata na Mitaa ya ZINGIZIWA zigawanywe zizaliwe Kata zingine Ili wananchi waweze kupata huduma za Jamii karibu na makazi wasitembee umbali mrefu .
Mwenyekiti Mpate alisema Kata ya Zingiziwa kwa Sasa ina Mitaa minane ya Chama na Serikali yote imekuwa changamoto ya ukubwa na umbali hivyo wapo Tayari kupokea maelekezo kwa ajili ya kutekekeza .
DIWANI wa Kata Zingiziwa Maige Maganga alipongeza Madiwani wa Halmashauri ya Jiji kwa ushirikiano wao Pamoja na Meya wao ndio Chachu ya Maendeleo ya Zingiziwa mpaka Sasa imekuwa ya kisasa .
DIWANI Maige alisema Kata ya Zingiziwa wamefanikiwa kupata pochi la mama limejenga madarasa 36 shule ya Sekondari pamoja na kituo Cha Afya Zingiziwa pia wamefungua Hospitali ya Zogoali Ms Zahanati ya Nzasa zote ni Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kazi inayofanywa na Rais wa Jamhuri ya MUUNGANO wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Pia DIWANI Maige alisema sekta elimu Zingiziwa wamepiga hatua kubwa shule ya Msingi Gogo kwa sasa imebadiishwa imekuwa English Medium kwa ajili ya kuwarahisishia Wazazi wa Zingiziwa watoto wao wasome eneo la makazi yao wasiende Daimond na Okimpio
Mwisho.