Home BUSINESS SERIKALI YALIPA MILIONI 40 ZA KIFUTA JASHO KWA WANANCHI KONDOA MJINI

SERIKALI YALIPA MILIONI 40 ZA KIFUTA JASHO KWA WANANCHI KONDOA MJINI

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imelipa kiasi cha shilingi milioni 40 ikiwa ni kifuta jasho/machozi kwa wananchi 198 wa Vijiji vya Chemchem, Tungufu, Tampori, Mulua na Iyoli wilayani Kondoa kutokana na kupata madhara yaliyosababishwa na wanyamapori.

Hayo yamesemwa Leo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kondoa Mjini, Mhe. Ally Juma Makoa aliyetaka kujua wananchi walioharibiwa mazao yao na tembo na kuhakikiwa watalipwa lini kifuta jasho/machozi.

Amesema Wizara ya Maliasili na Utalii ilifanya uhakiki wa madai ya kifuta jasho/machozi tarehe 25 hadi 28 Septemba,2022 kwa wananchi 274 wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa walioharibiwa mazao yao na tembo lakini baada ya uhakiki wananchi 198 ndio waliolipwa.

Aidha, amesema Wizara inaendelea kufanyia kazi malipo ya kifuta jasho/machozi ya wananchi waliowasilisha madai mapya.

Previous articlePEPFAR IMEPUNGUZA MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU TANZANIA-MAJALIWA
Next articleMWENYEKITI MTEMVU AMETOA BARAKA KUGAWANYWA KATA NA MAJIMBO ILALA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here