KOCHA Msaidizi wa kikosi cha Simba Seleman Matola amesema kuwa baada ya timu kufika nchini Morocco kikosi kitakuwa na siku tatu za maandalizi kabla ya mchezo wao dhidi ya Rs Berkane utakaopigwa jumapili usiku majira ya huku ni saa nne.
Matola amesema baada ya kufika jijini Casablanca kikosi kitafanya mazoezi ya utimamu wa mwili(recovery)kwa sababu tangu wamalize mchezo dhidi ya Us Gendarmerie Nationale hakijapata muda wa kupumzika vizuri.
Matola amesema kikosi kitaweka kambi ya muda Casablanca kabla a kwenda mji wa Berkanw ambapo mchezo wao utachezwa.
“Tubamshukuru Mungu tumefika salama Morocco kikosi kitafanya mazoezi ya utimamu wa mwili kwa sababu kwa siku mbili hatujafanya mazoezi tuna siku tatu za kujiandaa kabla ya mchezo” amesema matola