Home BUSINESS DKT. KIJAJI AKUTANA NA VIONGOZI WENZAKE KUPANGA MIKAKATI SIKU YA TANZANIA MAONESHO...

DKT. KIJAJI AKUTANA NA VIONGOZI WENZAKE KUPANGA MIKAKATI SIKU YA TANZANIA MAONESHO YA EXPO 2020 DUBAI

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (Mb.) (kulia) akiwa na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe. Bw. Omar Shaaban(Mb.) (Kushoto), Februari 23, 2022, Dubai ameongoza kikao cha maandalizi ya Siku ya Kitaifa ya Tanzania itakayofanyika 26/02/2022 wakati wa Maenesho ya EXPO2020 Dubai ikifuatiwa na Kongamano la Biashara na Uwekezaji ambalo litafanyika tarehe 27 Februari, 2022 ambapo Mgeni Rasmi wa Siku hiyo na Kongamano hilo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Siku hiyo, iliyoandaliwa kwa kushirikiana na Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) itafanyika wakati wa Maenesho ya EXPO2020 yaliyoanza 1 Oktoba, 2021 hadi 31 Machi, 2022 ambapo Tanzania ni miongoni mwa nchi 192 zinazoshiriki Maonesho hayo. Katika siku hiyo, Rais Samia anatarajia kufanya mazungumzo na Uongozi wa Serikali ya UAE kwa lengo la kukuza mahusiano ya kiuchumi na kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili na kutangaza fursa za uwekezaji na vivutio vya utalii.

Aidha, Kongamano litakalofanyika litahudhuriwa na Wafanyabiashara kutoka Tanzania, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na nchi Washiriki wa EXPO2020 Dubai.

Kongamano hilo litakutanisha Wawekezaji, Wauzaji na Wanunuzi wa bidhaa mbalimbali, na Taasisi za Kimataifa za Fedha katika jukwaa moja. Serikali ya Tanzania inatarajia kunadi Miradi ya Kimkakati kutoka Sekta za Viwanda, Kilimo, Madini, Utalii, Nishati, Miundombinu, Uchumi wa Buluu, Mawasiliano, Ujenzi, Afya, Uchukuzi na Elimu.
 
Tanzania inatumia fursa ya Maonesho hayo kutafuta masoko ya uhakika na endelevu ya bidhaa zitokanazo na mazao ya kimkakati kama vile kahawa, korosho, chai, mkonge, karafuu, pareto, viungo, mwani, nyama, Samaki na bidhaa nyingine zinazohitajika kwenye soko la kimataifa.

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) (Kushoto) akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi yaRais, Kazi na Uwekezaji, Mhe. Mudrick Ramdahan Solaga (Kulia) pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Godius Kahyarara (Katikati) Februari 23, 2022 wakati wa kikao cha maandalizi ya Siku ya Kitaifa Tanzania itakayofanyika 26/02/2022 ikifuatiwa na Kongamano la Biashara na Uwekezaji ambalo litafanyika tarehe 27 Februari, 2022.

Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma M. Rajabu akielezea hatua za maandalizi Februari 23, 2022 wakati wa kikao cha maandalizi ya Siku ya Kitaifa Tanzania itakayofanyika 26/02/2022 ikifuatiwa na Kongamano la Biashara na Uwekezaji ambalo litafanyika tarehe 27 Februari, 2022.


Kamishina Generali wa Banda la Tanzania kwenye Maonesho ya Expo2020 Dubai Mhe. Balozi Mohamed Mtonga akielezea hatua za maandalizi Februari 23, 2022 wakati wa kikao cha maandalizi ya Siku ya Kitaifa Tanzania itakayofanyika 26/02/2022 ikifuatiwa na Kongamano la Biashara na Uwekezaji ambalo litafanyika tarehe 27 Februari, 2022.
 
Previous articleYASEMAVYO MAGAZETI ASUBUHI YA LEO ALHAMISI FEBRUARI 24-2022
Next articleMATOLA: KIKOSI CHA SIMBA KIPO IMARA KUIVAA RS BERKANE J.PILI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here