Home LOCAL WASIMAMIZI WA ELIMU WAKUTANA KUJADILI MIPANGO YA KUBORESHA ELIMU SHINYANGA

WASIMAMIZI WA ELIMU WAKUTANA KUJADILI MIPANGO YA KUBORESHA ELIMU SHINYANGA

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bw. Moses Chilla akifungua Kikao Kazi cha Mapitio ya Tathmini ya Utekelezaji wa Shughuli za Uboreshaji na usimamizi wa elimu Mkoa wa Shinyanga kwa mwaka 2022 na Mpango wa mwaka 2023 kwa niaba ya Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Angellah Kairuki leo Ijumaa Januari 20,2023.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Wasimamizi Wakuu wa Elimu Mkoani Shinyanga wamekutana na kufanya Kikao Kazi cha Mapitio ya Tathmini ya Utekelezaji wa Shughuli za Uboreshaji na usimamizi wa elimu Mkoa wa Shinyanga kwa mwaka 2022 na Mpango wa mwaka 2023.

Kikao hicho kilichohudhuriwa na Maofisa Elimu ngazi ya mkoa na Halmashauri sita za mkoa, Maafisa Elimu kata wote, wakuu wa shule za msingi na sekondari, Wathibiti Ubora wa shule, Tume ya Utumishi ya walimu na Wakurugenzi wa Halmashauri kimefanyika leo Ijumaa Januari 20,2023 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Savannah Plains Manispaa ya Shinyanga.

Akifungua Kikao hicho kwa niaba ya Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Angellah Kairuki, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bw. Moses Chilla amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya maboresho makubwa katika sekta ya elimu ikiwemo elimu bure, kujenga shule, madarasa mapya hali inayosababisha idadi ya wanafunzi kuongezeka shuleni.

“Serikali imeendelea kuboresha sekta ya elimu na tunafarijika kuona mafanikio makubwa katika ufaulu wa wanafunzi, serikali itaendelea kuboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji”,amesema Chilla.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bw. Moses Chilla.

Aidha amewataka wasimamizi wa elimu kuhakikisha wanadhibiti mdondoko wa wanafunzi shuleni inayosababishwa na wanafunzi kutopata chakula, utoro na mambo mengine.

“OR TAMISEMI inaekeleza kila kiongozi wa elimu afuatilie ujifunzaji na ufundishaji shuleni ili kuongeza ufaulu. Kila mwalimu na kiongozi yeyote ahakikishe wanafunzi wanapata chakula shuleni”,amesema Chilla.

“Pia ni lazima kuwe na ulinzi kwa watoto shuleni, tuwasimamie watoto wetu kwani wanapata matatizo kwa sababu ya kukosa ulinzi. Lakini tufundishe nidhamu kwa wanafunzi, wanafunzi waongee lugha zenye staha na tusisahau kuwafundisha uzalendo wa kitaifa, tuwafundishe kuhusu tunu za taifa”,ameongeza Chilla.

Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Bi. Dafroza Ndalichako amezitaja baadhi ya changamoto zinazokabili sekta ya elimu mkoani Shinyanga ni pamoja na baadhi ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kuzifikia shule za kata, upungufu wa walimu na shule nyingi kutotoa huduma ya chakula kwa wanafunzi shuleni ambapo mkakati uliopo sasa ni kila shule huduma ya chakula kwa wanafunzi ili kuongeza utulivu wa wanafunzi, ufanisi na ufaulu kwenye mitihani.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi Elimu ya Awali na Msingi OR-TAMISEMI, Suzana Nussu kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, anayeshughulikia Elimu Dkt. Charles Msonde ameonya wasimamizi wa elimu kuepuka kuchanganya elimu na siasa.

“Tusichanganye siasa na elimu,msilete siasa kwenye mambo ya kitaalamu kwani haya mambo ndiyo yanatuvuruga kwenye sekta ya elimu. Pia baadhi ya walimu tunafanya dhambi, wakuu wa shule ingieni darasani muone jinsi walimu wanavyofundishwa”,amesema Nussu.

Ametumia fursa hiyo kuwaomba walimu kukaa na watoto ili kubaini changamoto zinazowakabili kwani dunia imebadilika watoto wanafanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia.

“Walimu fuatilieni mienendo ya wanafunzi wenu, hivi mtoto aliyelawitiwa usiku mzima huko nyumbani ataweza kuelewa unachofundisha darasani?, hivi mtoto anayerudi nyumbani anafanywa mke na mjomba wake atakuelewa kweli unachofundisha darasani?..wazazi nanyi muwe makini, fuatilieni mienendo ya watoto.

Nendeni mkatenge muda wa kuzungumza na wanafunzi, fuatilieni mienendo ya wanafunzi, kama vitendo vya ukatili havipo shuleni,basi  matukio hayo yapo mtaani, yapo nyumbani  kwani binadamu wamebadilika kuwa wanyama….Toeni taarifa ili tusiharibu watoto na kama kuna mwalimu anafanya matendo ya hovyo kwa watoto aache mara moja ”,amesema Nussu.

Wasimamizi wakuu wa elimu mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.

“Wale wenye shule za bweni imarisheni ulinzi mabwenini, wafuatilieni vizuri, na nyinyi kama wazazi kaeni na watoto wasikilizeni, watawaambia mambo mengi tuchukue hatua mapema”,amesema.

“Wafundisheni watoto mila na desturi za mtanzania, msiwalee watoto kama mayai, kuna baadhi ya shule binafsi zinaharibu sana watoto wetu, watoto wanashindwa hata kuosha vyombo”,ameongeza. 

 Ametumia fursa hiyo kuwaomba wanasiasa wanapofanya mikutano yao wahimize watoto kwenda shule huku akisisitiza umuhimu wa shule zote kuwapatia chakula wanafunzi wawapo shuleni na kuhakikisha wanafunzi wanaandikishwa shule na wote wanamaliza shule.

Naye Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi amewataka walimu na wazazi kulinda watoto huku akiwataka walimu kuacha kula mahindi ya shule (kufanya mapenzi na wanafunzi).

“Walimu wenye tamaa acheni kula mahindi ya shule, waacheni wasome, walindeni ili watimize ndoto zao,na mwalimu atakayebainika anakula mahindi ya shule atashughulikiwa”,amesema Chambi.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bw. Moses Chilla akifungua Kikao Kazi cha Mapitio ya Tathmini ya Utekelezaji wa Shughuli za Uboreshaji na usimamizi wa elimu Mkoa wa Shinyanga kwa mwaka 2022 na Mpango wa mwaka 2023 kwa niaba ya Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Angellah Kairuki leo Ijumaa Januari 20,2023. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bw. Moses Chilla akifungua Kikao Kazi cha Mapitio ya Tathmini ya Utekelezaji wa Shughuli za Uboreshaji na usimamizi wa elimu Mkoa wa Shinyanga kwa mwaka 2022 na Mpango wa mwaka 2023 kwa niaba ya Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Angellah Kairuki leo Ijumaa Januari 20,2023.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bw. Moses Chilla akifungua Kikao Kazi cha Mapitio ya Tathmini ya Utekelezaji wa Shughuli za Uboreshaji na usimamizi wa elimu Mkoa wa Shinyanga kwa mwaka 2022 na Mpango wa mwaka 2023 kwa niaba ya Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Angellah Kairuki leo Ijumaa Januari 20,2023.
Mkurugenzi Msaidizi Elimu ya Awali na Msingi OR-TAMISEMI, Suzana Nussu akizungumza kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, anayeshughulikia Elimu Dkt. Charles Msonde kwenye Kikao Kazi cha Mapitio ya Tathmini ya Utekelezaji wa Shughuli za Uboreshaji na usimamizi wa elimu Mkoa wa Shinyanga kwa mwaka 2022 na Mpango wa mwaka 2023

Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Bi. Dafroza Ndalichako akizungumza kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, anayeshughulikia Elimu Dkt. Charles Msonde kwenye Kikao Kazi cha Mapitio ya Tathmini ya Utekelezaji wa Shughuli za Uboreshaji na usimamizi wa elimu Mkoa wa Shinyanga kwa mwaka 2022 na Mpango wa mwaka 2023

Wasimamizi wa elimu wakiwa Kikao Kazi cha Mapitio ya Tathmini ya Utekelezaji wa Shughuli za Uboreshaji na usimamizi wa elimu Mkoa wa Shinyanga kwa mwaka 2022 na Mpango wa mwaka 2023

Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi akizungumza kwenye Kikao Kazi cha Mapitio ya Tathmini ya Utekelezaji wa Shughuli za Uboreshaji na usimamizi wa elimu Mkoa wa Shinyanga kwa mwaka 2022 na Mpango wa mwaka 2023

Wasimamizi wakuu wa elimu mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye Kikao Kazi cha Mapitio ya Tathmini ya Utekelezaji wa Shughuli za Uboreshaji na usimamizi wa elimu Mkoa wa Shinyanga kwa mwaka 2022 na Mpango wa mwaka 2023
Wasimamizi wa elimu wakiwa Kikao Kazi cha Mapitio ya Tathmini ya Utekelezaji wa Shughuli za Uboreshaji na usimamizi wa elimu Mkoa wa Shinyanga kwa mwaka 2022 na Mpango wa mwaka 2023
Wasimamizi wa elimu wakiwa Kikao Kazi cha Mapitio ya Tathmini ya Utekelezaji wa Shughuli za Uboreshaji na usimamizi wa elimu Mkoa wa Shinyanga kwa mwaka 2022 na Mpango wa mwaka 2023

Wasimamizi wa elimu wakiwa Kikao Kazi cha Mapitio ya Tathmini ya Utekelezaji wa Shughuli za Uboreshaji na usimamizi wa elimu Mkoa wa Shinyanga kwa mwaka 2022 na Mpango wa mwaka 2023
Wasimamizi wa elimu wakiwa Kikao Kazi cha Mapitio ya Tathmini ya Utekelezaji wa Shughuli za Uboreshaji na usimamizi wa elimu Mkoa wa Shinyanga kwa mwaka 2022 na Mpango wa mwaka 2023
Wasimamizi wa elimu wakiwa Kikao Kazi cha Mapitio ya Tathmini ya Utekelezaji wa Shughuli za Uboreshaji na usimamizi wa elimu Mkoa wa Shinyanga kwa mwaka 2022 na Mpango wa mwaka 2023
Wasimamizi wa elimu wakiwa Kikao Kazi cha Mapitio ya Tathmini ya Utekelezaji wa Shughuli za Uboreshaji na usimamizi wa elimu Mkoa wa Shinyanga kwa mwaka 2022 na Mpango wa mwaka 2023 
Walimu wakitoa burudani kwenye Kikao Kazi cha Mapitio ya Tathmini ya Utekelezaji wa Shughuli za Uboreshaji na usimamizi wa elimu Mkoa wa Shinyanga kwa mwaka 2022 na Mpango wa mwaka 2023
Wasimamizi wakuu wa elimu mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye Kikao Kazi cha Mapitio ya Tathmini ya Utekelezaji wa Shughuli za Uboreshaji na usimamizi wa elimu Mkoa wa Shinyanga kwa mwaka 2022 na Mpango wa mwaka 2023
Previous articleBARAZA LA TAIFA LA MICHEZO ZANZIBAR
Next articleKUNA ONGEZEKO LA ZAIDI YA TANI 70,000 ZA SUKARI NCHINI – DKT.ASHIL
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here