Home LOCAL WAZIRI NAPE AKIKAGUA UJENZI WA JENGO LA OFISI YA WIZARA MTUMBA

WAZIRI NAPE AKIKAGUA UJENZI WA JENGO LA OFISI YA WIZARA MTUMBA

.

Idara ya Habari – MAELEZO

Ujenzi wa jengo la Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari unatarajiwa kukamilika Oktoba 2023 hivyo kuongeza ufanisi wa wizara hiyo katika kuwahudumia Watanzania.

Akizungumza leo jijini Dodoma baada ya kukagua ujenzi wa jengo hilo linalojengwa katika Mji wa Serikali – Mtumba, waziri wa wizara hiyo, Mhe. Nape Nnauye amesema atatoa ushirikiano pale ujenzi utakapokwama.

Nimekuja kutembelea baada ya kuona kasi ya ujenzi inapungua, nataka kasi iongezeke," ameelekeza Mhe. Nape.

Pamoja na hilo, Msimamizi wa Mradi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Mhandisi Grace Musita amesema ujenzi ulitakiwa kukamilika Aprili 2023 lakini umechelewa kutokana na changamoto mbalimbali ikiwamo ugumu wa ardhi, kupanda kwa gharama za ujenzi na kuchelewa kupata michoro ya miundombinu ya mfumo wa majitaka.

“Mradi ulianza kutekelezwa mwaka 2021 kwa gharama ya shilingi bilioni 23.9, tumeshalipwa shilingi bilioni 7.9 tu, ujenzi umefikia asilimia 59.5 na tumefwata taratibu zote za ujenzi kwa kupima vifaa vyote vya ujenzi” ameeleza Mhandisi Musita.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi wa Jengo, Ndg. S.H Mvunye amesema jengo hilo litakuwa na muonekano wa ghrofa tano na moja ya chini (basement).

Previous articleCCM YATOA AGIZO KUHUSU WALIMU KUPEWA VISHIKWAMBI
Next articleRAIS WA ZANZIBAR ALHAJ DK.HUSSEIN MWINYI AJUMUIKA NA WANANCHI KATIKA IBADA YA SALA YA IJUMAA MASJID NOUR MUHAMMAD KWAMCHINI UNGUJA LEO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here