Home BUSINESS SIDO YASHIRI MAONESHO YA NANENANE KITAIFA JIJINI MBEYA

SIDO YASHIRI MAONESHO YA NANENANE KITAIFA JIJINI MBEYA


Na: Hughes Dugilo, MBEYA.

Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) limetoa mwito kwa wajasiriamali hususani wanaojihusisha na kilimo na bidhaa za usindikaji kujihepusha na watu wanaotoa mafunzo mitaani na badala yake kufika katika vituo vya SIDO vilivyoeneoa nchi nzima ili kupata mafunzo sahihi na kuweza kufikia malengo yao kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora.

Akizungumza katika mahojiano maalum katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya, Meneja Masoko wa SIDO Lilian Massawe amesema kuwa lengo la wao kushiriki katika maonesho hayo ni kutoa fursa kwa wananchi kupata elimu juu ya teknolojia ya viwanda vidogo itakayowawezesha kupata tija katika shughuli zao.

Amesema kuwa katika maonesho hayo wamekwenda na wahjasiriamali mbalimbali waliopata mafunzo kupitia Shirika hilo na kwamba wananchi wanakaribishwa kutembelea katika banda hilo.

TAZAMA VIDEO HAPA.

https://youtu.be/6zi0W_ZGagk

Previous articleBoT KATIKA MAONESHO YA NANENANE JIJINI MBEYA
Next articleNIC: MIFUGO ILIYOKATIWA BIMA KUTAMBULIWA NA KIFAA MAALUM
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here