Home BUSINESS BRELA YAWAPIGA MSASA WAFANYABIASHARA ELIMU YA MILIKI UBUNIFU

BRELA YAWAPIGA MSASA WAFANYABIASHARA ELIMU YA MILIKI UBUNIFU

Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Miliki Ubunifu wa BRELA Bwa. Seka Kasera akizungumza na waandishi wa habari katika semina ya wafanyabiashara Jijini Dar es Salaam. 

Badhi ya washiriki wa Semina hiyo wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Miliki Ubunifu wa BRELA Bwa. Seka Kasera (hayumo pichani) alipokuwa akitoa mada katika semina hiyo.

Afisa Mwandamizi Idara ya Miliki Ubunifu- BRELA Raphael Mtalima katika semina hiyo

Baadhi ya watumishi wa BRELA wakiwa katika semina hiyo.

(PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, DSM.

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umetoa mwito kwa wafanyabiashara nchini kulinda alama zao za biashara sambamba na kulinda  bidhaa zinazozalishwa nchini na kwa kufanya hivyo watakuwa wamelinda uchumi  wa nchi yao.

Akizungumza katika semina ya siku moja iliyoandalwa na wakala huyo iliyofanyika leo Januari 19, 2022 Jijini Dar es Salaam iliyolenga kuwajengea uelewa wafanyabiashara hao, Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya miliki ubunifu wa BRELA Bwa. Seka Kasera, amesema kuwa endapo wafanyabiashara wataelimika katika kulinda  bidhaa zinazozalishwa nchini watakuwa wamelinda uchumi wa Taifa.

“Unapolinda bidhaa zinazozalishwa nchini unalinda uchumi wa Taifa, hivyo wafanyabiasha wanapaswa kutumia na kuzilinda alama zao za Biashara” amesema Kasera.

Ameongeza ili nchi iweze kusonga mbele ni lazima technojia itumike hasa kulinda alama zao (Logo) itakayowawezesha kulinda bidhaa zao na kupunguza migogoro ya kuiga alama ya mtu mwingine.

“Kuna wengine hawazipi kipaumbele alama zao za biashara hivyo kwa kongamamo hili wafanyabiasha watapata mafunzo ili wazipe kipaumbele ‘Logo’ zao”

Ameongeza kuwa anaamini mafunzo hayo yatakwenda kuwaongezea uwezo katika uzalishaji wa bidhaa bora na zenye viwango vya kimataifa na kwamba mafunzo hayo yatasambazwa nchi nzima.

“Mafunzo haya yatasambazwa nchi nzima hasa kwa Wafanyabiasha wadogo wadogo ili wote waweze kupata mafanikio kwenye soko la kimataifa na kuweza kuongeza thamani katika bidhaa zao” amesema Bw. Kasera.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo Martin Mbwana na Agripina Thomas wameishukuru BRELA kwa kuwapatia mafunzo hayo na kwamba wanaamini elimu hiyo itawawezesha kuzalisha bidhaa zenye ubora zaidi.

Previous articlePRUDENCIA PAUL KIMITI ATEMBELEA NA KUTOA MSAADA VITUO VYA KULELEA WATOTO YATIMA NA WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU RUKWA.
Next articleBALILE: WADAU WANA SHAUKU KUONA MUSWADA SHERIA YA HABARI UKISOMWA BUNGENI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here