Home Uncategorized PRUDENCIA PAUL KIMITI ATEMBELEA NA KUTOA MSAADA VITUO VYA KULELEA WATOTO YATIMA...

PRUDENCIA PAUL KIMITI ATEMBELEA NA KUTOA MSAADA VITUO VYA KULELEA WATOTO YATIMA NA WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU RUKWA.

Prudencia Paul Kimiti ametembelea na kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali katika vituo vya kulelea Watoto yatima vya Peter’s House Bangwe na Katandala Orphanage Center.

Kituo cha kwanza alichotembelea ni kituo cha Peter’s House kilichopo Kata ya Izia mtaa wa Bangwe ambapo katika kituo hicho Prudencia alitoa vifaa vya shule kwa wanafunzi ambao wanasoma shule mbali mbali za serikali na binafsi wanaosomeshwa na kituo hicho.

Amekabidhi madaftari ya kuandikia na Ma counter books kumtosha kila mwanafunzi, kalamu za wino, kalamu za risasi na mikebe na alitoa Juice, Mchele na kuacha pesa za kununulia nyama ili watoto waweze kula na kufurahi kwa pamoja kama watoto wengine wanaoishi kwa wazazi wao.

Kituo cha pili alichotembelea ni kituo cha watoto yatima cha katandala yaani Katandala Orphanage Centre kinachopatikana Kata ya Katandala ambapo Katika kituo hicho Prudencia alitoa msaada wa maziwa kwa watoto wachanga, mkaa wa kupikia na kuacha pesa ya kulipia bili ya umeme.

Aidha, alifarijika sana kuona wanafunzi wote wanaosoma katika vituo vyote viwili kuwa na uwezo mkubwa wa kitaaluma katika masomo yao, na alipowahoji baadhi yao walimueleza kuwa wanasoma kwa bidii ili waweze kuwa madaktari na wengine Wanajeshi ili kuisaidia nchi na watu wake hapo baadae.

Hata hivyo, Prudencia anatoa rai kwa wadau wa ustawi na maendeleo jamii Mkoa wa Rukwa kuendelea kushirikiana na vituo hivi ambavyo vinalea watoto waliobeba ndoto za kuisaidia nchi siku za usoni.

Pia, anawapongeza TRA Sumbawanga kwa kuwa karibu kusaidia mahitaji muhimu ya mara kwa mara katika kituo cha Peter’s House.

Previous articleKAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA WIZARA YA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA KWA UTENDAJI KAZI WAKE
Next articleBRELA YAWAPIGA MSASA WAFANYABIASHARA ELIMU YA MILIKI UBUNIFU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here