Home LOCAL WAZIRI UMMY: SEKTA YA AFYA ITAENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA UTENGAMAO NA KUWAWEZESHA...

WAZIRI UMMY: SEKTA YA AFYA ITAENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA UTENGAMAO NA KUWAWEZESHA WALEMAVU KUMUDU MAISHA.



Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiongea katika hafla ya kukabidhi viti mwendo, miguu bandia, bima za afya na fimbo za kutembelea kwa wasiona jiji Arusha

Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini Mrisho Gambo akiongea katika hafla ya kukabidhi viti mwendo, miguu bandia, bima za afya na fimbo za kutembelea kwa wasiona.


NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema sekta ya afya wataendelea kuboresha huduma za utengamao nchini ili kuwa na takwimu sahihi za mahitaji ya watu wenye ulemavu katika kuwawezesha waweze kumudu maisha kwa kutumia viungo alivyonavyo.

Waziri Ummy aliyasema hayo katika hafla ya kukabidhi miguu bandia ,viti mwendo,bima ya afya na fimbo za kutembele watu wasioona ambapo  alisema kuwa huduma za utengamao zinajumuisha huduma tiba za mazoezi ya viungo,kuzungumza na tiba kwa vitendo.

“Huduma hizo ni pamoja na kutengeneza vifaa tiba visaidizi na nyinginezo katika ngazi zote za utoaji wa huduma za afya hivyo nakiri kuboresha huduma za utengamao na ninahaidi watu wote wenye ulemavu nchini watahakikisha wanapata takwimu sahihi za mahitaji halisi ya huduma  za utengamao,”alisema Waziri Ummy.

Mwalimu alisema kuna viashiria vinavyoonyesha uhitaji mkubwa  wa huduma za utengamao kwa watu wenye ulemavu ambapo watu hao wenye uhitaji hutoka kwenye makundi tofauti tofauti wakiwemo watu wenye magonjwa mbalimbali, watu wenye ulemavu na umri mkubwa pamoja na waliozaliwa na ulemavu.

Waziri alisema kutokana na sensa mwaka 2012 inaonyesha watu wenye ulemavu inaonyesha asilimia ya 5.8 ya Watanzania walikuwa na tatizo la ulemavu ambao wanaweza kuwa na mahitaji ya huduma hizo za vifaa tiba kwa hiyo walionyesha asilimia ya wazee ni 3.8 ambao pia wanahitaji huduma hizo za utangamao.

Naye Mbunge wa jimbo la Arusha mjini,Mrisho Gambo alisema amewashukuru wadau mbalimbali kujitokeza katika kuwasaidia baadhi ya vifaa tiba kwa watu wenye ulemavu wa wilaya ya Arusha kwani sio kitu rahisi.

Pia alisema alimshukuru Rais wa jamuhuri ya Muungano Tanzania Samia Suluhu Hassani kuwa mstari wa mbele katika katika kuwahudumiwa wananachi na kusikiliza changamoto zao.
“Nitaendelea kushirikiana na serikali pamoja na viongozi mbalimbali kuhakikisha tunatatua changamoto za wananchi kwa lengo la kuleta maendeleo,”alisema Gambo Mbunge wa Arusha mjini.

Naye Mwenyekiti wa watu wenye ulemavu wilaya ya Arusha,Martha Mganga alisema anamshukuru mbunge huyo kwa kuwasaidia vifaa tiba mara tatu mfululizo limekuwa jambo la kihistoria kwao ambapo ni takribani jumla ya vifaa tiba hivyo ni 247 na bima za afya 100.

Mwisho.
Previous articleMARTIN KADINDA AWAPA NENO WANAWAKE NA VIJANA WAJASIRIAMALI KISIWANI ZANZIBAR
Next articleARUSHA: WAZIRI UMMY AKIPONGEZA KITUO CHA SANAA TANZANIA KWA KUWAPA WALEMAVU AJIRA.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here