Papa wa zamani Benedict XVI amefariki dunia katika makazi yake Vatican, akiwa na umri wa miaka 95, karibu muongo mmoja baada ya kujiuzulu kwa sababu za kiafya.
Papa Benedict aliongoza Kanisa Katoliki kwa muda usiozidi miaka minane hadi, mwaka 2013, akawa Papa wa kwanza kujiuzulu tangu Gregory XII mwaka 1415.
Benedict alitumia miaka yake ya mwisho katika monasteri ya Mater Ecclesiae ndani ya kuta za Vatican.
Siku ya Jumatano, Papa Francis alitoa wito kwa hadhira ya mwisho ya mwaka huko Vatican “kusali sala maalum kwa ajili ya Papa Emeritus Benedict”, ambaye alisema alikuwa mgonjwa sana.