Home SPORTS YANGA YAFIKISHA ALAMA 50 LIGI KUU YA NBC, YAILAZA MTIBWA SUGAR...

YANGA YAFIKISHA ALAMA 50 LIGI KUU YA NBC, YAILAZA MTIBWA SUGAR 1-0

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara timu ya Yanga imeendelea kujishindilia kileleni mwa msimamo wa Ligi hiyo kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Katika mchezo huo uliopigwa leo Disemba 31,2022 kwenye uwanja wa  Manungu Turiani, Morogoro timu ya Yanga ilipata bao katika dakika ya 26 ya mchezo huo, goli likifungwa na Stephanie Azizi Ki kwa mpira wa adhabu uliomshinda mlinda mlango wa Mtibwa Sugar.

Katika kipindi cha pili cha mchezo huo timu zote zilionekana kushambuliana ambapo katika dakika ya 77 ya mchezo huo timu zote zilifanya mabadiliko huku Yanga ikiingiza wachezaji watatu  na Kagera Sugar ikiwaingiza washambuliaji wawili Onesmo Mayaya na Joseph Mkele.

Hata hivyo mabadiliko hayo hayakuweza kuzaa matunda kwa timu ya Mtibwa Sugar na kufanya kutoka uwanjani wakiwa wamekubali kichapo cha bao 1-0.

Kufuatia ushindi huo timu ya Yanga imeendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa Ligi ya NBC Tanzania Bara kwa kuwa na alama 50 wakizidi kumuacha mpinzani wake wa karibu Simba SC yenye alama 44.

Previous articlePAPABENEDICT  WA XVI AFARIKI DUNIA
Next articleDAWASA YAWATAKIA KHERI YA MWAKA MPYA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here