Na: Mwandishi Wetu, GEITA.
Naibu Waziri Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari *Mhe. Mhandisi Kundo Andrea Mathew* ameonyesha kufurahishwa na mikakati ya Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Geita. Akizungumza katika kikao kazi cha Viongozi na watendaji wa Mkoa wa Geita kuhusu operesheni Anwani za makazi kilichofanyika ijumaa tarehe 18,March 2022 amesema;
“Hakuna mbadala wa zoezi la Mfumo wa Anwani za makazi ni lazima tuhakikishe tunalikamilisha kwa namna yoyote ile kwakufanya hivyo tutawezesha ufanisi katika zoezi la Sensa ya watu na makazi litakalofanyika August 2022 ikiwa ni maono ya Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kuleta maendeleo na kutoa huduma kwa uwiano wa idadi ya watu katika eneo husika..”
“Nimefurahishwa sana na mikakati ya Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huu. Tumemsikia Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Geita Ndg. John Wanga wametenga Milioni mia moja na Ishirini (Tshs. 120,000,000/=) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Geita Bi.Zahara Michuzi amesema wametenga kiasi shilingi Milion Mia moja na kumi (110,000,000/=) Hii ni ishara njema sana.”