Home LOCAL GEITA WAMKOSHA NAIBU WAZIRI KWA KUTEKELEZA ZOEZI LA MFUMO WA ANWANI ZA...

GEITA WAMKOSHA NAIBU WAZIRI KWA KUTEKELEZA ZOEZI LA MFUMO WA ANWANI ZA MAKAZI.

Na: Mwandishi Wetu, GEITA.
Naibu Waziri Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari *Mhe. Mhandisi Kundo Andrea Mathew* ameonyesha kufurahishwa na mikakati ya Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa  Geita. Akizungumza katika kikao kazi cha  Viongozi na watendaji wa Mkoa wa Geita kuhusu operesheni Anwani za makazi kilichofanyika ijumaa tarehe 18,March 2022 amesema;

 “Hakuna mbadala wa zoezi la Mfumo wa Anwani za makazi ni lazima tuhakikishe tunalikamilisha kwa namna yoyote ile kwakufanya hivyo tutawezesha ufanisi katika zoezi la Sensa ya watu na makazi litakalofanyika August 2022 ikiwa ni maono ya Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kuleta maendeleo na kutoa huduma kwa uwiano wa idadi ya watu katika eneo husika..”


“Nimefurahishwa sana na mikakati ya Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huu. Tumemsikia Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Geita Ndg. John Wanga wametenga Milioni mia moja na Ishirini (Tshs. 120,000,000/=) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Geita Bi.Zahara Michuzi amesema wametenga kiasi shilingi Milion Mia moja na kumi (110,000,000/=) Hii ni ishara njema sana.”

Previous articleNGWANDO, KIBAZANGE KUGOMBANIA UBINGWA PST KESHO CHAMPION KITAA
Next articleMAKAMU WA RAIS DKT.MPANGO AMUWAKILISHA RAIS KATIKA IBADA YA SHEREHE YA JUBILEI YA DHAHABU YA MIAKA 50
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here