Na: Farida Mangube, Morogoro.
Idadi ya vifo vitokanavyo na ajali maeneo mbalimbali ya migodini hapa nchini imepungua kwa kiasi kikubwa tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma kutoka vifo 106 idadi liyoripotiwa mwaka 2018 hadi kufikia 33 kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni.
Hayo yalisemwa na Katibu Mtendaji Tume ya Madini Mhandisi Yahya Samamba kwenye kikao kazi wakaguzi wa migodi na baruti nchini kilichofanyika mkoani Morogoro ambapo alisema mbali na idadi ya vifo kupungua pia idadi ya matukio ya ajali nayoimepungua kutoka 43 hadi kufikia 16.
“Hapo nyuma matukio ya ajali migodini yalikuwa kwa wingi sana,kwa mwaka 2018 matukio ya ajali ambayo yaliripotiwa yalikuwa 63 na katika matukio hayo vifo vilikuwa ni 106,watu waliopata ulemavu walikuwa 43,tumefanya kazi kubwa ili kuhakikisha matukuo ya ajali na vifo vinapungua”alisema Yahya.
Katibu huyo alimpongeza Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira pamoja na wakaguzi wote wa tume ya madini kwa kitendo cha kuchukua hatua ambayo imeweza kusaidia kupunguza matukio ya ajali na vifo migodini.
Alisema matukio ya ajali midogoni kwa wachimbaji wakubwa na wakati yapo kwa kiasi kidogo tofauti na wachimbaji wadogo wa kwani ndiyo hawanga wakubwa wa ajali hizo na hiyo ni kwa sababu na uduni wa teknolojia wanazozitumia wao.
“Mara nyingi wachimbaji hao hutumia matimba na kwamba matimba hayo yasipopangwa vizuri,kuwa imara,yakitumika muda mrefu huoza na kusababisha mashimo ambayo huwafukia ndugu zetu ambao ni wachimbaji”alisema Yahya.
Aidha alitaka matumizi mazuri ya baruti ili kuepuka kuathiri kwenye jamii zinayozunguka migodi ambapo aliwataka wakaguzi kuhakikisha suala hilo la baruti linatumika vizuri pamoja na kuweka takwimu za matumizi na pia kuhakikisha wote wanaohusika na baruti wanakuwa na vibali.
Kwa upande wake Mkaguzi Mkuu wa Migodi ambaye pia Mkurugenzi wa Ukaguzi Migodi na Mazingira Mhandisi Henri Nditi alisema kuwa semina hiyo itawapa ari na nguvu mpya wakaguzi wa migodi katika kutekeleza majukumu yao.
Alisema kwenye uchimbaji wa madini ili uwe endelevu lazima kuwe salama,kusiwe na ajali na pia mazingira yatunzwe kwa manufaa ya kizazi cha sasa na cha baadaye na kwamba semina hiyo ni muhimu sana katika kukuza sekta ya madini nchini.
Kwa upande wake mshiriki wa semina hiyo Mhandisi Gabriel Senge alisema katika kikao kazi hicho na mafunzo hayo washiriki wanatarajia kujifunza mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati ya kuendeleza na kusimamia usalama katika migodi,utunzaji wa baruti ili kuongeza tija katika uzalishaji madini.