Home BUSINESS NMB YAZINDUA HUDUMA YA WAKALA KWA SIMU ZA MKONONI

NMB YAZINDUA HUDUMA YA WAKALA KWA SIMU ZA MKONONI

Afisa Mkuu wa wateja binafsi na Biashara, Filbert Mponzi, kulia kwake Kaimu Mkuu wa Uthibiti hatari na utekelezaji, Oscar Nyirenda , Afisa Mkuu wa teknolojia na mabadiliko ya kidigitali, Kwame Makundi na Mkuu wa idara ya bidhaa, Aloyse Maro (wa pili kushoto) Meneja mwandamizi chaneli za huduma, James Manyama.

Benki ya NMB imezindua huduma maalumu ya kuweka na kutoa pesa kirahisi kupitia wakala watakao tumia simu zao za mkononi tu. 

Huduma hiyo ya NMB Pesa Wakala imezinduliwa jijini Dar es Salaam, ikilenga kusogeza ‘Karibu Zaidi’ huduma za kifedha kwa wananchi, pamoja na kutoa fursa za ajira kwa Watanzania, lengo likiwa kuongeza idadi ya mawakala kutoka 11,000 wa sasa, hadi 100,000 miaka mitano ijayo. 

Huu ni muendelezo wa utoaji wa suluhishi za kidijitali zilizo rahisi na salama kwa wateja ili kuwafanya kuendelea kufurahia huduma zao popote walipo.

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi, alivitaja vigezo vya mtu kuomba uwakala wa NMB Pesa Wakala kuwa ni pamoja na Leseni ya Biashara, Kitambulisho cha Taifa (NIDA) na simu ya mkononi ya aina yoyote (smartphone au kitochi). 

Sasa Wakala anaweza kutumia huduma hii kupitia simu yake ya mkononi tu, bila kuhangaika kupata mashine za PoS ambazo zinatumia kadi. Kwa mteja, hakikisha umejiunga na NMB Mkononi kuweza kufurahia huduma hii kiurahisi.

Previous articleKAMISHNA JENERALI WA DCEA ASHIRIKI KIKAO CHA WAKUU VYOMBO VINAVYOHUSIKA MAPAMABANO YA DAWA YA KULEVYA NCHINI AFRIKA KUSINI
Next articleSERIKALI IMEDHAMIRIA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI – WAZIRI UMMY MWALIMU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here