Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Balozi. Dkt. Pindi Chana, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Patrobas Katambi pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Njombe wakifuatilia vijana wa halaiki wakiwa wanafanya mazoezi ya mandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe , tarehe 31 Machi, 2022,
Vijana wa halaiki wakiwa wanafanya mazoezi ya maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe tarehe 31 Machi, 2022, Mbio hizo zitazinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Philip Isdor Mpango tarehe 02 Aprili, 2022.
Vijana sita walioandaliwa kutoka Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, watakaokabidhiwa jukumu la kuukimbiza Mwenge wa Uhuru katika Mikoa 31 na Halmashauri 195 za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa siku 195, wakiwa katika maandalizi ya Uzinduzi wa mbio hizo tarehe 02 Aprili, 2022.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Balozi. Dkt. Pindi Chana, (katikati) akifuatilia maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe, kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa Njombe, Waziri Kindamba na kushoto kwake ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Patrobas katambi, wengine ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Prof. Jamal Katundu pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Bi. Fatma Rajabu.
Mkurugenzi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Idara ya Maendeleo ya Vijana, Bw. Julius Tweneshe akitoa ufafanuzi juu ya maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe, tarehe 02 Aprili, 2022.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)