Home LOCAL SERIKALI KUHAKIKISHA DAWA ZA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA KUWEPO KWENYE VITUO VYOTE NCHINI

SERIKALI KUHAKIKISHA DAWA ZA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA KUWEPO KWENYE VITUO VYOTE NCHINI




Na: Catherine Sungura,WAF-Dodoma

Serikali itahakikisha dawa na vifaa tiba  za magonjwa yasiyoambukiza zinapatikana kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kote nchini.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichalwe wakati wa kufunga mafunzo kwa  ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza kwa watoa huduma za afya kutoka mikoa nane Tanzania bara yaliyofanyika jijini Dodoma.

Dkt. Sichalwe amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya imechua hatua mbalimbali katika kupambana na magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo ya utekelezaji wa mkakati jumuishi wa III wa kuzuia na kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza 2021/2026.

“Mkatati huu unahuisha kuhakikisha watoa huduma  wanapewa mafunzo ili waweze kutoa huduma  bora za magonjwa yasiyoambukizwa kote nchini katika ngazi zote za utaji  huduma  za afya”.

Dkt. Sichalwe aliwataka washiriki hao kuwafundisha  watoa huduma za afya waliopo  katika mikoa wanayotoka ili kutimiza azma  ya Serikali  na hivyo kuchangia  katika kuboresha  nguvu kazi  ya Taifa inayotegemea wananchi wenye afya njema.“Jitihada  zozote zenye kusaidia mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukia zinaendelea kuungwa mkono na sisi wenyewe’ Alisisitiza.

Aidha, Mganga Mkuu wa Serikali aliwataka watoa huduma hao kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi wote ili watu wachukue tahadhari na kuepuka na magonjwa hayo au magonjwa hayo kutowaathiri zaidi na hivyo wanapaswa kuwashirikisha Viongozi kuanzia ngazi ya kitongoji,kijiji,mtaa na kata.

Hata hivyo alitoa rai kwa wananchi kuacha tabia bwete na hivyo kuchuchua tahadhari ya kuepuka magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo Kisukari,Moyo  na mengine na kuhimiza kufanya mazoezi, kula mlo kamili na kuacha kutumia vileo kupita kiasi pamoja na kuacha matumizi ya tumbaku.

Dkt. Sichalwe ametoa rai kwa wadau wengine wa maendeleo kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutoa mafunzo mbalimbali katika sekta ya afya ili kuboresha huduma za afya na kukishukuru Chama cha Kisukari Tanzania(TDA) kwa kuwezesha mafunzo hayo kwa mikoa ya Kigoma, Lindi, Singida, Songwe, Arusha, kilimanjaro, Dodoma na Mara.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za  Tiba kuyoka Wizara ya Afya Dkt. Omary Ubuguyu amewakumbusha watoa huduma hao kuchukua historia ya mgonjwa anapofika kwenye kituo cha afya ili kuweza kutoa matibabu sahii.

-MWISHO-

Previous articleSERIKALI KUSIMAMIA SERA ZINAZOHUSU LISHE NCHINI
Next articleABSA TANZANIA YAHAMASISHA WATANZANIA KUCHANJA CHANJO YA COVID-19
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here