Wanafunzi 191 wa kidato cha pili Wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita hawajafanya mtihani wa taifa wa kidato cha pili Wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita Jamhuri Wiiliam ameagiza kukamatwa kwa wazazi wa wanafunzi hao ambao hawajafanya mtihani wa kidato cha pili kutokana na utoro ili wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.
Jamhuri ameswma wilaya hiyo itafanya Msako wa nyumba kwa nyumba utakaoenda sambamba na kuwakamata wanafunzi watoro na kuwarudisha shuleni.
“Hili jambo limetushitua nimeagiza Mkurugenzi, afisa elimu watendaji wa vijiji na kata watoto hawa wasakwe popote walipo warudishwe shuleni na isiishie kwao wazazi wao wakamatwe wapelekwe kwenye vyombo vya sheria ili iwe fundisho kwa wengine”
Afisa elimu sekondari wa halmashauri hiyo Patrick Atanas amesema sababu kubwa zinachangia changamoto hiyo ni pamoja na mimba za utotoni,mwamko mdogo wa wazazi kuhusu elimu,shughuli za migodi,ufugaji na kilimo.
“Wapo wazazi wanawalazimisha watoto wafeli ili wasiendelee na shule upande mwingine wanafunzi wanashida wenyewe hawapendi kusoma sisi kama idara ya elimu tunachofanya ni kuwaelimisha waone umuhimu wa elimu wawekeze kwenye masomo”.